Sunday 19 November 2006

Maji ya Dezo yafikia kikomo Zenj...

Baraza la Wawakilishi hatimae kwa shingo upande limepitisha mswaada wa kulipia huduma ya maji katika visiwa vya zenj. Hii ina maana kuwa ile kauli ya "maji ya Karume(maji ya bure)" inafikia kikomo. Wananchi wa visiwa hivyo wamekuwa wakitumia maji bure tokea mwaka 1964. Gharama zote za matumizi ya maji zilikuwa chini ya serikali hivyo kufanya sekta hiyo kwa kiasi fulani kudumaa na hasa baada ya Azimio la Zanzibar, ambapo Visiwa hivyo vilishuhudia ongezeko kubwa la mahitaji ya maji.

Wafadhili kadhaa kwa wakati tofauti waliishauri SMZ kubadili mfumo wake ili kuweza kupatikana kwa huduma bora ya maji bila mafanikio.

Hata hivyo kutokana na shida kubwa ya maji, na kuanzishwa kwa sustainable programme kupitia NGO na CBO Baadhi ya wananchi walianza miradi ya kujitafutia maji ya bomba kwa gharama zao wenyewe. Miradi hii imekuwa ya mafanikio sana kwao.

Nina matumaini makubwa kuwa wafadhili ambao walisusa kuanzisha mfumo mpya wa ugawaji maji katika visiwa vyenye maji safi na matamu duniani nzima(nunua Drop kama huamini), watarudi na kuendeleza shughuli zao pale walipoachia.

Kwa upande mwingine wananchi wa Zenj wawe tayali kukubali kulipia maji na kutumia maji kwa uangalifu na zaidi kutunza huduma hiyo.
Hii ni kwa faida yetu wenyewe, vilevile kutawezesha huduma hiyo kuwa endelevu. Tukumbuke kuwa Hudumu ya maji ni Kwa faida yetu sisi wananchi na ni wakati wetu kusimamia hudumu hiyo ili iweze kuwa endelevu.

No comments: