Sunday 19 November 2006

SMZ siku zote inanichekesha

Hivi karibuni SMZ imefuta kiwanja cha ubalozi wa Oman kwa madai ya kuwa kipo sehemu mbaya kiusalama! eti kipo karibu sana na beach!

Mwee! hivi nani hasa huwa anaomba kiwanja?
Nijuavyo mimi ni kuwa Taasisi au mtu binafsi huomba Kiwanja kwa kutaja sehemu ambayo huona ni muafaka kwake kuwa na kiwanja. Hivyo nina amini kuwa ubalozi wa Oman uliomba kiwanjwa hicho kwa kuwa wao waliona kuwa eneo hilo ndio linafaa kwako kujenga ofisi ya ubalozi na sio sehemu nyingine yoyote ile. Na SMZ wakati ule iliridhia kutoa kiwanja hicho kwa ubalozi wa Oman, licha ya kwenda kinyume na maelekezo ya masterplan ya hifadhi na uendelezaji wa Mji Mkongwe.

Hata hivyo Ubalozi haukujengwa zaidi ya eneo hilo kuzungushiwa ukuta tu ambao kwa kiasi fulani ulikuwa ni kero tupu kwa watu ambao walikuwa wanaegesha magari katika eneo hilo... Zaidi kuzuia sehemu ya kuanzia kwa mashindano ya ngalawa.

Leo hii SMZ kama kawa imeibuka na kusema kuwa eneo hilo halifai kwa ujenzi wa ofisi ya ubalozi, kwa sababu za kiusalama?

Usalama wa aina gani ambao SMZ wanaosema?... Ikulu ipo beach, Hospitali kuu ipo beach, Mahakama Kuu ipo beach, ubalozi wa Misri upo beach.. yaani kila ofisi muhimu hapo zenj zipo beach! sasa ni kwanini tu Ubalozi huo usiwe beach?
Kama mmefuta umiliki wa uwanja huo kwa ajili ya kubadilisha matumizi ya ardhi kwa kiwanja hicho, itakuwa ni jambo la busara iwapo kiwanja hicho kitarudishiwa matumizi yake ya awali kama eneo wazi.

Kuwepo kwa ukuta katika eneo hilo kwa kiasi fulani kulizorotesha sana maendeleo ya kibiashara kwa maeneo ya karibu kama vile Starehe Club, Wings, Garage Club, n.k

No comments: