Wednesday, 16 May 2007

Wazenj wa UK na Vituko Vyao...

Nilipofika hapa UK yapata mwezi sasa, nilikuwa na hamu kubwa ya kukutana na watz wanaishi huku, zaidi kuonana wa Wazenj wa huku ili niweze kubadilishana nao mawazo kuhusu vituko, vioja na kadhia kadha wa kadha za huko Zenj.
Well haikuwa kazi kubwa kabisa kuwatafuta wazenj, kwani nilipofika mwenyeji wangu alikuwa ametingwa sana na kazi zake za kila siku, hivyo alinitaka radhi kuwa hataweza kunipikia chakula cha jioni. "nikahisi sasa ndio kuna kulala na njaa" Hata hivyo alinitoa hofu kuhusu kupata kwa msosi, kwa kuniambia kuwa tayali ameshatoa oda ya msosi, ambao anahisi kuwa utanifaa na kunikumbusha huko bongo, na hasa katika soko la usiku la chakula huko Zenj(Forodhani).
Muda si mrefu tokea kuingia ndani kwa mwenyeji wangu, chakula cha jioni kikaletwa! MMhm nikaamini maneno yake, kwani ulikuwa ni msosi ambao nimeukasa kwa muda mrefu sasa... Chapati, samaki waliokaangwa kwa viuongo rukuki vya kisiwani, mchuzi mzito maandanzi, na mazagazaga mengine kibao.. ile harufu yake ilipofika puani mwangu, mate kibao yalijaa mdomoni. Baada ya kufakamia msosi ule wa jioni, mwenyeji wangu aliniambia kuwa umetoka kwa Wazenj ambao wao wamefungua mgahawa bubu wa kupika vyakula kwa order.
Asubuhi yake niliamua kuingia mitaani kuangalia hili na lile, baada ya kutembea tembea bila dira maalumu nilijikuta naingia kwenye sehemu ya kukatia nywele. Hapo niliamua kupunguza nywele zangu. Hata hivyo kulikuwa na watu wengi, hivyo nikabidi kusubiri. Vinyozi walikuwa kama wanne hivi wakiendelea na kazi zao... baadae walianza kuongea kwa lugha ya kiswahili yenye rafudhi ya mwambao, nikahisi hapana shaka watakuwa ni Wazenj, hivyo nikajiweka sawa kuwasikiliza. Hata nafasi ya kunyolewa ilipopatikana nilikaribishwa kwa lugha ya Kiingereza... mimi nikajibu kwa lugha ya Kiswahili. Nikanyolewa huku tukiongea hili na lile na hasa mambo ya Zenj. Nilipomaliza nikawauliza sehemu ambayo ninaweza kukutana na Watz wengi kwa wakati mmoja. Wakanielekeza.
Ni jioni, nikaamua kwenda kutembelea sehemu ambayo nitakutana wa Watz wengi kwa wakati mmoja. Ni baa maridadi kabisa na ya kisasa. Nilipoingia ndani ilikuwa imejaa watu kibao wa kila rangi. Baa ya kuchukua bia yangu, nikaanza kutafuta sehemu nzuri ya kukaa. Nikaona bora nokae karibu na meza moja iliyokuwa imejaa weusi kibao amboa walionekana wakifurahia vinywaji vyao ipasavyo. Nilipoangalia vizuri meza hiyo nikaona kuna kijana ambae niliwahi kuishi nae Malaysia ambae ni Mzenj. Nikamwita na kumkumbusha, kwani alionekana kunisahu. Baada ya kunikumbuka alinikaribisha kwa furaha tele kwenye meza yao. Akanitambulisha kwa rafiki zake, ambapo niligundua kuwa wote ni kutoka Zenj...Baada ya glass mbili hivi nikamuuliza kama kuwa Watz wa bara katika baa hiyo. Akanionyesha kwa kidole kuwa wamekaa kule... Well nikamwambia wacha nikawasalimu nao pia.
Baada ya kukaa kwa Wabongo kwa muda kadhaa nikahisi kuwa kuna kitu kinaendelea kati ya Wazenj na Wabongo... kwani ninapotoka sijawahi kuona utengano wa aina hii. Well sijui ni nani aliyeanzaa. Ila kwa haraka haraka nikahisi kuwa ni Wazenj ambao walikuwa na vituko ambavyo vimepelekea kuwepo na utengano huu... Hata hivyo nitazidi kuchimbachimba ili nijue vituko vyao.....

3 comments:

SIMON KITURURU said...

Duh!Mzee unanikumbusha mitaa ya kwa rafiki zangu wa Kikuyu na Waluo .Kuna sehemu nilikatiza nakusikia mambo mpaka baadhi wanafikiria kununua bunduki.Kisa kikubwa ni sehemu tu walizotoka zinazoanzisha mushkeli.
Tuletee zaidi basi!Usihukumu kabla ya kufikia ukoko kuwa nani kaanza.Ila noma utengano

Anonymous said...

Watanzania wa visiwani wanapenda kujitenga sana sijui ni kwanini.Nimesoma nao walikuwa hivyo hivyo.

jimjaam said...

Eleza baa gani ueenda? na kwa kigezo gani umechukua kugundua hao wazenji ndio matatizo? mimi niko hapa London miaka kumi na saba na nimeenda sehemu nyingi tofauti na naona watu wanashirikiana kwa mambo yote, misiba, socializing,nk acheni fitina za kijinga izo!!!!