Thursday 14 June 2007

Mahakama Kuu ni Kimeo....

Nimewahi kuandika kuhusu mashaka makubwa ya mahakama za zenj katika mabandiko yaliyopita, leo hii kumeibuka kadhia nyingine ambayo hapana shaka ipo kwa muda mrefu tu huko zenj..

Imeripotiwa kuwa mahakama za zenj, hasa Mahakama Kuu haina majaji wa kutosha hivyo kukosa hadhi ya kuitwa Mahakama Kuu kwa mujibu wa katiba ya visiwa hivyo. Tatizo la Majaji huko visiwani lipo kwa muda mrefu sana, ingawa kuna wakati smz ilijitia kifua mbele kwa kukodisha majaji toka nje ya visiwa hivyo(Mapopo).

Kwa mwananchi wa kawaida hawezi kuamini kuwa Visiwa hivyo havina majaji, kwani wao mtu yoyote afanyae kazi mahakamani basi ni jaji, kama ilivyokuwa katika hospitali zao kwa wafanyakazi wote huitwa ni madokta.

Pengine ujuha huu wa kushindwa kutofautisha mgawanyiko wa ngazi za wafanyakazi, upo ndani ya vibosile wa SMZ kiasi cha kujisahau kuwa hawana Majaji wa kutosha kuendesha kesi lukuki katika Mahakama Kuu. Udhaifu wa mahakama za zenj na hasa katika watendaji wake umekuwa ni gumzo kubwa katika kipindi hiki, wakati kuna fufunu ya uteuzi wa Jaji Mkuu mpya wa Tanzania,

Ukiachana na hayo ambayo yanatia kichefuchefu, Mahakama ya Mkoa wa Mjini Magharibi ina Mahakimu watatu tu, ambao kwa maneno mengine ndio Mahakimu wa Mikoa yote ya Zanzibar! kwani sio siri kuwa sijawahi kusikia Hakimu wa Mikoa mengine minne wakitajwa, licha ya kesi walizohukumu kuripotiwa...! Hao Mahakimu wa wilaya wapo kwa hesabu ya vidole, na wengi wao wapo katika Mahakama za wilaya ya Mjini na ile ya Magharibi... Nasikia huko Pemba kuna mahakama ya Mkoa vilevile, hata hivyo Hakimu wake kutwa yupo Vuga!

SmZ kupitia kwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali wanapaswa kuja na suluhisho la kudumu kuhusu kadhia hii, na sio kila siku kuwa ni watetezi wa uchovu wa SMZ. Iwapo wao ndio wanasimamia Mahakama na sheria zake, basi hawana budi kuwa na mipango madhubuti ili kuona kuwa vyombo vya haki visiwani humu vimekamilika kwa mujibu wa sheria na katiba ya visiwa hivyo. Kitendo cha kuwaondoa Wapopo katika Mahakama zetu kilikuwa kizuri kwa manufaa ya watu na uchumi wetu unaodorola, aidha ipo haja basi ya ofisi hiyo kupanda Jahazi hadi bara ili kupata Majaji wenye kujua sheria zetu na maadali ya Mtanzania.

5 comments:

Simon Kitururu said...

Kazi kweli kweli!

Aliko said...

hivi judge uchaguliwa au anahitaji shule ya namna fulani kusikilia huo wadhifa huo?

Anonymous said...

mimi ni mzanzibari na ninasoma sheria hivi shahada ya pili sasa nategemea baada ya miaka michache niombe kuwa judge.tatizo sio smz haina majaji bali ni lazma watu wasome ili kuwa jaji wananchi wenyewe wanatakiwa wafungue macho especially vijana vijana ili wawe majaji na hii ndio solution ya kila nchi,huwezi kumuokota muuza majchungwa ukamuweka mahakamani kuwa jaji ni lazima mtu aelimike kwa kiwango kinachokubalika kuwa jaji, serikali yenyewe ingeweka msisitizo wa kusomesha vijana na vijana nina imani wapo wengi tuu ila hawana uwezo na serikali inafanya ubahili kuwasomesha .

Simon Kitururu said...

Che,nime kutag.
Tujulishe vitu nane tusivyojua kuhusu wewe.

Kibunango said...

Simon:
Nitavitaja baada ya wewe kuniambia vitu nane unavyojua kuhusu mimi...
Cheers!