Wednesday 29 August 2007

Kauli ya Nahodha ina Walakini

Waziri Kiongozi wa Zenj, ambae yupo mkoani Ruvuma ametoa kauli ya kusisitiza kuwa, Elimu ndio njia pekee ya kuwaletea maendeleo wakazi wa Mkoa huo,kutokana na mkoa huo kukosa Umeme wa kuhaminika na kuwa na barabara mbovu. Msisitizo wa kauli hiyo aliutoa kwa kufananisha ukuaji wa kasi wa uchumi wa Singapore na udodoraji wa maendeleo ya mkoa huo na Tanzania kwa ujumla.

Kauli hii ina utata mkubwa kwani elimu pekee haiwezi kuleta maendeleo yoyote iwapo njia zingine za kuleta maendeleo zitakuwa zimebanwa kwa wananchi. Mkoa wa Ruvuma unasifika kwa kuzalisha Mahindi, Kahawa, Tumbaku,Alizeti na mazao mengine. Kabla ya mwaka 1984, usafiri wa kwenda huko ulitegemea zaidi njia ya anga (ATC).Usafiri wa barabara ulikuwa ni wa usumbufu mkubwa na uliweza kuchukua muda mrefu kufika mkoani. Kufunguliwa kwa barabara ya Makambako - Songea katika kiwango cha lami, kulitoa fursa kubwa kwa mkoa huo kuvuma katika uzalishaji wa Mahindi. Barabara hii haikuja kutokana na elimu ya waakazi wa huko bali ni kutokana na umuhimu mkubwa wa taifa kupata Mahindi na Kahawa toka mkoani huko.

Mkoa wa Ruvuma kwa miaka mingi umekuwa ukitegemea umeme wa nguvu ya jenereta, ambao licha ya kuwa ni ghali kuuendesha, upatakanaji wake umekuwa ni wa kimgao kwa zaidi ya miaka ishirini sasa. Sasa hapa sijui elimu ya aina gani inatakiwa ili mkoa huo uunganishwe kwenye gridi ya taifa, ambayo inapita katika mikoa ya jirani zake.

Nimeshindwa kuelewa kauli ya Nahodha, kati ya kuwa na elimu na uwewezeshaji wa miundo mbinu na uchumi wa mkoa husika. Kwa mfano majumba ya michenzani huko Zenj hayakujengwa kwa kuwa waakazi wa zenj wote walikuwa ni wajuzi wa ujenzi. Yalijengwa kwa sababu uchumi wa Zenj kipindi hicho ulikuwa unaruhusu, na viongozi kwa kushirikiana na wananchi waliona upo umuhimu wa kufanya hivyo.

Kwa mkoa wa Ruvuma kuwaambia kuwa tatizo lao la umeme litatatuka kwa kuwa na elimu na sawa na kuwaondoa njiani tu...

4 comments:

Simon Kitururu said...

Umenikumbusha mbali! Maswala ya kwenda Ruvuma kabla ya barabara ya lami; Ule mlima wa lukumbulu na ufinyanzi wake , yale magari ambayo unakuta yamekwama masiku kibao njiani, hapo achana na yale uyaonayo pembeni ya barabara yamepinduka!Ndege za ATC vilevile zile nyingine zenye nyufa ndani!Kusafiri na ndege za jeshi za mizigo!Kweli Ruvuma ilikuwa kazi! Nilikuasijui kuwa mpaka sasa Ruvuma inatumia genereta za mafuta.DUH!

Kibunango said...

Sawasawa Hiyo ndio ilikuwa Ruvuma.. Shurti upitie Lukumbulu...
Hata hivyo Kwa wasiojua inakuwa ni vigumu kuelewa.

Aliko said...

Ruvuma ni mkoa wa kipekee kwanza kabisa kiutamaduni wagoni ni mfano mkubwa wakuigwa hawa jamaa niwatuzaji wazuri wa mila na desturi mpaka leo hii utaona baadhi ya elements za kizulu ktk ngoma,uimbaji nk kumbuka hawa ni maimmigrants toka kusini mwa Afrika,kwa kilimo hawa jamaa ogopa walijulikana kama zebig five miaka ya nyuma kabla ya wale wataalamu feki wa kilimo kuintroduce mbolea ya kichumvichumvi ambayo ni husika kwa uharibifu mkubwa ardhi nchini.
kuwambia hawa jamaa kwamba wanahitaji elimu iliwaendelee si makosa ila ni elimu gani haswa wanaihitaji ilo ndio swala maake elimu ni matumizi serikali inahitaji kuwekeza katika rasimali nyinginezo za kiuchumi,naelimu inayotakiwa ni ile ambayo itamufaisha na kumwezesha mwananchi kwani sio siri kilimo tuu siku hizi sio uti wamgogo kama zamani, kuna mhe mwingine katoa hoja hivi majuzi katika shule moja ya nimrod mkono,kwamba vijana wafundishiwe kichina ati kwasababu uchina inaendelea kwa kasi ......sio lazima viongozi kutoa hotuba kila watembeleapo mikoa mara nyingine wawewasikilizaji tuu watajifunza mengi na wataheshimika zaidi.

Simon Kitururu said...

@Kibunango:Kweli kabisa kwa ambao hawakupitia hii kitu ni vigumu kulielewa hili jambo.
@Altunez:Kweli kabisa jambo hili. Lakini Viongozi wetu wanafikiri kuwa kuongea na ahadi za uongo ndio ujanja.Kumbe wakati mwingine kusikiliza ndio ujanja.