Friday, 8 February 2008

Lowassa Ajiwekea Rekodi Zake...Siku ya jana imeingia katika kumbukumbu za serikali na maelfu ya wananchi wa Tz na wengine wenye uhusiano na Tz kwa namna moja ama nyingine.

Katika kuangalia angalia habari ya Lowassa nimekuja kufahamu kuwa ndie Waziri Mkuu wa kwanza kujiuzuru kutokana na tuhumu ambazo nimemgusa moja kwa moja tokea mwaka 1961. Hii ni rekodi kwake na rekodi ya kumbukumbu kwa viongozi wa ngazi za juu ambao kwa namna moja ama nyingine walijiuzuru, pasipo kuwa na tuhumu zinazowakuga wao Binafsi...

Kama vile haitoshi, Bw. Lowassa ameweka rekodi nyingine mpya ya kuwa kiongozi wa juu kabisa kujiuzuru huku akitizamwa na kusikilizwa na maelfu ya Watanzania kupitia Television ya Taifa (TVT). Rekodi nyingine ambayo ameiweka hapo jana ni kujiuzuru mbele ya Bi. Lowassa. Kwa ufupi Bw. Lowassa amejiwekea rekodi kama tatu hivi katika kipindi kifupi kabisa katika historia ya kujiuzuru kwa viongozi hapo Tz.

Mbaya zaidi, ni kuweka rekodi ya kiongozi wa kwanza kujiuzuru muda mfupi kabla ya ziara ya Prezedent Bush, ambaye anatoka huko kulikosababisha Bw. huyo kujiuzuru. Pichani hapo juu ni picha ambayo inaonyesha mapenzi yake na nchi ya Prez. Bush, ambapo sasa anaweza kumwona kwa kupanga foleni kama wananchi wa kawaida.

7 comments:

EDWIN NDAKI said...

Haya kamanda nilipita kukusabahi.

Sikujua kama na wewe unajiblog.


aaa ,,inapendeza sana.

tuwekee na picha za Klubi basi tuzione.

wasalimie lile jengo mkabala na Klubi...aaa aaa

kibunango said...

Karibu sana Kamanda...

Anonymous said...

Sasa blog ya stori za zenji kwa nini unaanza kukosea kiswahili kwenye utangulizi tu!? badilisha hapo kisiwa KIMEJAALIWA sio kimejariwa we vipi!!!?

kibunango said...

anony:
Ndio vituko venyewe hivyo,aidha shukrani kwa kuona hilo

Anonymous said...

Embua acha kutumia picha fake. Wewe huoni kuwa inaonekana wazi kuwa ni fake ndugu yangu?

SIMON KITURURU said...

Sema Mkuu!Tuko Pamoja !

kibunango said...

Sawa Kamanda...