Monday 15 September 2008

Ngoma Afrika Band na Ziara yao Ulaya...









Bendi ya mziki wa dansi ya The Ngoma Africa inayoongozwa na mwanamziki nguli Ebrahim Makunja alimaarufu Ras Makunja hilifanikiwa kuufunga mtaa mrefu katikati ya jiji la mji mashuhuri wa Hamburg,katikati ya eneo maarufu hamburg-Haltona,
kulikuwa pata shika ya Nguo Kuchanika wakati bendi hiyo mashuhuri kwa kuwadatisha washabiki hakili na mziki wao wa dansi "Bongo dansi" kutoka Tanzania ukiwa unarindima
Live katikati ya mji katika tamasha kubwa la aina yake Afrika-Festival.

Hilikuwa majira ya saa 2.30 usiku wakali wa mziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa band walipanda jukwaani na kuanza kuporomosha nyimbo zao za kiswahili zilizo sindikizwa na mdundo mkali wa dansi ! mziki ambao uliweza kuwazoa mashabiki kwa kasi
ya aina yake na kuwatia kiwewe maelfu ya washabiki katika tamasha hilo.

*Ni Ras Makunja na Bendi ya The Ngoma Africa !
siku hiliyofuatia 30-08-2008 wakali wetu hawa walipanda jukwaa kubwa katikati ya
mji wa Krefeld,katika onyesho kubwa la wiki ya mwafrika (Africa Week) huko nako kuwa
patashika washabiki wamataifa mbali mbali wakiwa wamechanganyikiwa na mdundo wa
dansi wa Tanzania,jukwaa lilikuwa limezungukwa na walinzi wenye suti na miwani meusi,
Ras Makunja na kikosi chake wakiwa jukwaani na kuhakikisha mdundo huo unawamtingisha kila mtu.

Bendi hiyo ambayo imefanikiwa kuwanasa washabiki wa ulaya na mziki wao wa dansi
kutoka bongo Tanzania,inasemekana ndio bendi pekee ya mziki wa dansi iliyoweza kugusa hisia za kila mshabiki,si watoto wala wakubwa,vijana kwa wazee,wake kwa waume,wazungu na weusi hili mradi dansi lao linatingisha.

Taarifa hii imeletwa kwa hisani kubwa na Msema Kweli

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

hakuna kulala hata kama hujala haya mpaka lyamba

Kibunango said...

Hiyo mpaka Lyamba imenikumbusha mbali..!

Anonymous said...

Hawa jamaa ni wakali sio mchezo!
halafu wanajiamini sana

Aliko said...

Makunja na wenzake watakuwepo mwezi wa pili Jijini Tampere wakimsindikiza mzee wa reggae Tanzania JahKimbute.. mzee wa kibunango taarisha kamera yako.

Kibunango said...

Hii ni habari njema...