Wednesday, 28 January 2009

Walevi Tende kumbe wapo wengi...


Ziara ya Prez Kikwete kule PBA na Zenj ambayo imemalizika hivi karibuni, imeacha maneno mengi na hasa kutokana na hotuba zake ambazo alizitoa wakati wa ziara hiyo. Huku wengi akilidhika na yale yote ambayo alihutubia katika mikutano ya hadhara na wakati wa funguzi mbalimbali wa miradi, wachache wakiongozwa na chama cha maalim wameendelea kubeza kama kawaida yao.

Kwa upande wangu ziara hiyo ilikuja katika wakati muafaka kabisa na ni baada ya sherehe za Mapinduzi ambazo zinakumbuka Mapinduzi yaliyo zaa serikali ya walio wengi visiwani humo. Mapinduzi haya yalikuja mwezi mmoja baada ya Uhuru wa mashaka uliotolewa na Waingereza kwa Waarabu wachache na jamaa zao huko visiwani zikiwaacha wananchi walio wengi katika giza la kitwana. Historia ya mapinduzi hayo kwa sasa itakuwa inafahamika vizuri kwa kila mtanzania kwani imeshapita miaka 45 tokea yatokee na kila mwaka yamekuwa yakikumbukwa. Na hivi leo anapotokea mtu ama kikundi cha watu kuhoji ama kubeza mapinduzi hayo, inafaa umtizame mara mbili mbili kama tayali ameshapata vinibu kadhaa ama la!

Mwaka jana kuna kundi ambalo linadai kuwa linahusu Uhuru wa Zenj, ambalo liliamua kuadhimisha sherehe haramu za uhuru! Mpaka sasa sijajua walikusudia nini katika maadhimisho hayo, ingawa wao walikuwa na haya ya kusema

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiongozi maandalizi ya sherehe hizo, Daud Jabil Seif, alisema wameamua kuadhimisha sikukuu hiyo ili kuwaenza waasisi wa uhuru wa Zanzibar wa mwaka 1963 ambao hawakumbuliwi na serikali.


Sasa hii maana yake ni nini kama sio kuanzisha chokochoko dhidi ya Mapinduzi ya mwaka 1964. Hapana shaka kabisa huu ni ulevi wa tende toka katika mtaimbo wa kwanza. Kwa zaidi ya miaka 40 imekuwa ikielezwa maana ya mapinduzi ya Zenj na kwa nini yalifanyika na kwa nini yataendelea kudumishwa.

Walevi wengine wa tende wanajaribu kuingiza mfumo wa vyama vingi na hatima ya Mapinduzi ya Zenj. Wao huku macho yao yakiwa mekundu kutokana na ulevi wa tende na asusa za mapera mchana wa jua la utosini huku wakivuja mijasho wanasema kuwa
Lakini kauli ambayo nataka zaidi kwa leo kumhusisha nayo Rais Kikwete ni ile ya kulileta tena suala la Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 na kama kawaida linapotajwa suala hilo malaika huwasisimka watu. Alisema haiwezekani kabisa kuchezea Mapinduzi hayo ambayo sasa yana umri wa miaka 45.

"Kama hajipendi ajaribu…kama hajitaki ajaribu…Yote chezeeni Mapinduzi hapana…ukiyachezea Mapinduzi unawarudisha watu kwenye utumwa, unawarudisha watu kwenye utwana. Hili liliondoka Januari 12, 1964 na halitarudi tena….haiwezekani."Hiyo ndio kauli aliyoitoa Rais Kikwete ambayo inanifanya nijiulize masuala chungu nzima na hasa kuhusisha kauli hiyo na suala zima la demokrasia na ushiriki wa kisiasa hapa Zanzibar.


Mlevi huyu amesahau kuwa vyama vingi vimekuja baada ya Mapinduzi na vimeidhinishwa na Baraza la Wawakilishi ambalo ndio utunga sheria kwa serikali ya mapinduzi. Hapana shaka mlevi huyu ambae ni mwandishi wa makala kadhaa, bado ana faida za tende na kusahau kuwa Chama chochote cha siasa ambacho kitashindwa kuyatambua mapinduzi ya Zenj hakina nafasi ya kutawala huko Zenj. Maalim na madevu yake alijaribu mara kadhaa na joto lake ameliona na sasa amefyata mkia. Hata hivyo sio rahisi kuaminika kwani jamaa wale walipelekewa tu taarifa za Mapinduzi hivyo hawajui uchungu wake... Na Wengi wanajua kuwa Uchungu wa mwana aujuae mzazi

Pamoja na mambo mengine Prez JK aliwaambia waziwazi wale wote ambao wanabeza maendeleo ya SMZ na JMT katika visiwa hivyo ni sawa na walevi wa tende, kauli ambayo naona inawafaa sana maruuni hao.

2 comments:

Anonymous said...

Aslm'Alykm!
Ahsante ndugu Kibunango.... Nimetembelea blog yako nikaona japo niwache salamu.

Kila la kheri

XP

kibunango said...

Karibu sana XP....