Thursday, 12 February 2009

Ni wiki ya Sauti za Busara (Sounds of Wisdom) huko ZanzibarTamasha la sita la Sauti za Busara limeshaanza rasmi siku ya Jana kwa maanandamo ya ufunguzi wa tamasha hilo ambalo sasa ni mojawapo ya tamasha kubwa kabisa barani Afrika. Tamasha hili litadumu kwa muda wa siku sita(12-18/02/2009)na tokea kuanza kwake limekuwa likifanyika katika wiki ya pili ya mwezi wa pili.

Tamasha la mwaka huu litatumbuizwa na wasanii maarufu toka karibu pande zote nne za Afrika, kwa mjibu wa tovuti ya sauti za busara wasanii ambao wana washabiki wengi kwa mwaka huu ni Bi Kidude, Culture Musical Club, DJ Yusuf, Samba Mapangala & Orchestre Virunga, Jagwa Music, Best of WaPi, Iddi Achien'g, Natacha Atlas, Segere Original na Joh Makini

Kwa habari zaidi tembelea hapa chini

No comments: