Sunday, 26 April 2009

Muungano unazidi kukua, miaka 45 sio mchezo...


Katika kusherehekea miaka 45 ya Muungano nimejikuta nikikumbuka sana shoki shoki, matunda yenye radha ya aina yake ni maarufu sana hapo Zenj. Anyway lengo ni kusherekea muungano, miaka 45 sio mchezo! Muungano huu ambao ulizaliwa na mambo kumi na moja, sasa una mambo 38 na bado una kero ambazo kuchwa zinapigiwa kelele! Sasa cha kujiuliza muungano huu unakua au unapolomoka. Ukiangalia idadi ya mambo yanayounganisha nchi mbili hizi utaona kama unakua na kama unakuwa unaelekea upande gani? Kuunganisha kila jambo na kuwa na serikali moja?

Hata hivyo dalili zinaonyesha kuwa mengi kati ya hayo 38 yameingizwa kwa upande mmoja kuburuzwa na upande mwingine, ndio maana kumezaliwa neno kero za muungano! Kwa hali ya sasa dalili za kukua kwa muungano huu ni kidogo kuliko kukua kwa kero zake! Nini kifanyike? yarudishwe yale 11 ya mwanzo au haya ya sasa yajadiliwe kwa kina na kuondoa hizo kero. Je ni upande mmoja tu wa muungano ambao unaona kuna kero? na kama ni hivyo upande mwingine wa muungano unajisikia vipi kukaa kimya na kutosikiliza kero za upande mwingine? Ni kiburi ama dharau? Au kuna ajenda ya siri?

Nawatakiwa kila heri watanzania wote katika siku hii muhimu ya kuzaliwa kwa Tanzania.

1 comment:

EDWIN NDAKI said...

KIBUNANGO unajua kukua kama ulivyosema sio suala ambalo watu washerehekee kama vile kukua inamaana chanya tu..

Ndio maana darasani ukipata 90 chini ya mia unasherekea..yaani unafurahia ukubwa au wingi wa alama..lakini 90 hiyohiyo inaweza kuwa kero kubwa hasa pale darasani mpo 91 na wewe tena ukapa namba kubwa yaani 90 inamaana wewe ni wapili kutoka mwisho.

Ila kwa jinsi muungano unavyokwenda,umetekwa zaidi na utashi wa kiasiasa bila kuwafikiri wazalendo wa kawaida zaidi..
Binafsi ninahofu sana iwapo utafikisha miaka 50 kero nazenyewe zitakuwa 50 sasa hapo sijui safari itakuwaje?

Any way..tutafika tu