Tuesday, 30 June 2009

Leo ni siku kubwa kwangu....


Leo ni siku kubwa kwangu, na ni baada ya kumaliza masomo ya Mazingira katika ngazi ya Shahada... Hapa nipo njiani kwenda kuchukua Nondo yangu. Aidha kwangu mimi ni sehemu kubwa ya mafanikio yangu binafsi na jamii mbalimbali ambako nilijitolea wakati wote wa masomo yangu katika kukamilisha miradi yao.

Habari zaidi nitaziandika mara baada ya kukabidhiwa ramsi Nondo hii... Kwa wale ambao wapo Tampere na Helsinki mnakaribishwa kujumuika nami katika siku hii adhimu.

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

HONGERA SANA KAKA KIBUNANGO

kibunango said...

Ahsante Da' Yasinta... kama unaweza kuja fasta fasta karibu sana kushereheka nami!

cally said...

hongera wangu, wapi kupongezana leo? tuambizane sio kimya kimya, pia nasubiri copy ya hicho cheti hapa mtandaoni;)

kibunango said...

Dear, Cally..
Lunch imepita ilikuwa Ilves, vinywaji vinaendelea Passion hadi saa 11 jioni, kabla ya kuhamia Cafe Europa na baadae Grolia... Ni siku ndefu leo!
Karibu sana...:)

SIMON KITURURU said...

Hongera Sana Mkuu!

Anonymous said...

Kibs,

Mbona taarifa yenyewe imechelewa? Na siku yenyewe Jumanne imekaa kinoma noma.

HATA HIVYO,
Hongera sana tena sana!

MtiMkubwa.

kibunango said...

Simon na MtiMkubwa:
Shukrani sana! Aidha Mtimkubwa ndio hivyo tena siku haikuwa nzuri sana kwani ni mwanzo wa wiki... Anyway tutaonana Hlk weekend!

Anonymous said...

hongera sana kwa kumaliza masomo yako kwa mafanikio. Nakutakia mafanikio zaidi.

hua nafurahia michango yako kwenye jamii forums

Kaziyabure said...

kaka hongera sana tena sana,sana sana sana!