Tuesday 29 September 2009

Tahadhari:- Zanzibar kuna Kipindupindu...

UGONJWA wa kipindupindu umeua watu watatu Zanzibar, wengine 20 wamelazwa katika kambi maalumu, Mtopepo visiwani humo.

Ugonjwa huo ulililipuka juzi katika shehia ya Chumbuni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Mkurugenzi wa Afya ya Jamii wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Juma Rajab,amesema,wagonjwa 20 wanapatiwa matibabu katika kambi ya wagonjwa wa kipindupindu iliyofunguliwa juzi.

Ingawa Rajab hakuwa tayari kuelezea tukio hilo kwa undani, alisema wauguzi na madaktari wanajitahidi kukabiliana na ugonjwa huo na pia kuchunguza chanzo chake
.


Bw. Rajab, chanzo cha gonjwa hilo angalia hapa chini



1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Mara nyingi hili swala la kutupa taka limezungumziwa na watu huwa hwalitilii mkazo kwa hiyo sasa tunaona matokeo yake. Poleni sana wafiwa. Nafikiri Bwana afya ana kazi ya kuhamasisha watu wasitupe taka ovyo.