Tuesday, 26 January 2010

Maridhiano: Alichosahau Maalim Seif...


Maalim Seif katika taarifa yake ya Maridhiano na Mustakbali wa Zanzibar, amezungumzia mengi juu ya Zanzibar ilipotoka hadi ilipo sasa. Cha ajabu hakuzungumzia kabisa juu ya kuwepo kwa utumwa visiwani humo, kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.

4 comments:

mrfroasty said...

Sasa Maalim Seif azungumzie utumwa kwani hilo kongamano lilikuwa linajadili utumwa?

Anonymous said...

huyu alie-post hii picha bado hajatushawishani tuamini kama picha hii ni zanzibar, kwanza hapana pahala palipoandikwa kuwa hapa ni zanzibar, nikisema bagamoyo au mafia au kirwa nitakosea?
hii picha haioneshi chochote juu ya pahala fulani. jaribu kuwa makini ili watu wakuelewe, this picture doest not show any thing regarding place, except persons standing

Anonymous said...

ukweli zanzibar hapakuwepo na utumwa, wala hakuna mtu yoyote anaeweza kukwambia kuwa yeye babu yake aliuzwa zanzibar, au alikamatwa zanzibar na kuuzwa kama mtumwa ulaya ama kwangineko. nijuavyo mimi watumwa walikuwa wanakamatwa tanganyika na kupitishwa zanazibar kwa ajili ya kusafirishwa ulaya. na hii picha inaonesha huu ni mji wa kirwa kivinje uliopo tanganyika wakati huo na mimi nishatembelea hapa.

Anonymous said...

Kama wapo waathrika wa Utumwa si na wajitokeze! Waseme sisi ni ukoo uliotokana na dhulma ya utumwa Zanzibar hata kama sasa hivi anaishi nje ya Zanzibar.

Tatizo letu halikuwa ni juu ya Utumwa. Tatizo ni kwenye siasa wenyewe na wengine huonelea kusema kuwa ni chimbuko la migogoro ya tokea chaguzi za kabla ya Uhuru wa Zanzibar na baadaye Mapiduzi.

Bwana mweye blog, kwenye makala yako moja humu humu umegusia kuwa kabla ya haya maridhiano ambayo wewe unaita mapatano, kuwa Zanzibar kulikuwa na ubaguzi wa Pemba na Unguja. Kwenye makala yako hugusia habari ya Utumwa. Lakini hata huo wakati wa ubaguzi hukujitokeza kusema kama Zanzibar kuna ubaguzi, ulikaa kimnya na kuangalia manaufaa yako.

wakati huo wa Ubaguzi, CCM ilifika wakati ikawa inawaacha wasomi wa Kipemba na kutafuta wasomi wa CCM kutoka Bara kasababu CCM Zanzibar kwenye kusoma hawamo. Ndio mtu kama wewe ukaweza kupata ajira ambayo ilipaswa kupewa Mzanzibari.

Kama Maalim Seif hakuzungumzia ya Utumwa, jee Amani na Dr Shein wamezungumzia hilo la Utumwa? Dr Aman amealikwa mpaka US, mbona hakugusia hilo la Utumwa na huko ndiko haswa watumwa walipokuwa wakipelekwa?