Sunday 31 January 2010

Nampuzika kuingia JF


Kwa muda wa miaka minne nimekuwa nikishiriki kikamilifu katika forum ya Jamii(JF). Kwa muda wote nilipokuwa katika forum hiyo nimeweza kujifunza mengi sana katika suala zima la ujenzi wa Taifa letu.

Binafsi nina blog yangu hii ambayo kwa muda mrefu nimekua nikiangalia kadhia mbalimbali hasa zinazohusu SMZ na Jamii nzima ya Tz visiwani. Hata hivyo sikuwa mbele sana katika kuona blog hii ikishiriki kikamilifu katika ujenzi wa Zanzibar, hii ni kutokana na kuweka nguvu zangu nyingi Jamii Forums.

Michango yangu ndani ya JF ilihusu sana suala zima la Visiwani na hatima yake, JF kama ukumbi huru umeweza kutoa nafasi kubwa kwa washiriki wake kujadili kwa kina kadhia mbalimbali zinazo zorotesha maendeleo ya Tanzania. Aidha kwa upande wa visiwani JF imekeuwa ikiota nasafi kubwa kwa kupokea michango mbalimbali juu ya hatima ya siasa za visiwani. Kwa hili napenda kuwapongeza sana watendaji wa JF na wachangiaji wa mada hizo.

Mimi binafsi nimewahi kuwa mtendaji katika SMZ, na nimeweza kukamilisha majukumu kadhaa yenye lengo ya kuboresha maisha ya watu wa visiwani. Majukumu hayo niliweza kuyafanya katika kipindi ambacho siasa za ubaguzi zilikuwa juu sana. Ubaguzi ambao ninaongelea hapa ni kuhusu Pemba na Unguja. Hapana shaka maelfu ya wapenda siasa wanajua kuhusu hili.

Hatua iliyofikiwa mwaka huu ya kuondoa tofauti za kisiasa ni jambo la kujivunia sana. Kitendo cha Mhe Karume na Maalim Seif kukutana kwa ajili ya kuondoa tofauti za kisiasa baada ya kushindwa kwa miafaka kadhaa sio jambo la kukebehi, ila ni mwanzo kwa kujenga upya Zanzibar iliyopotea kwa miaka zaidi ya therathini.

Pamoja nakejeli nyingi alizotupiwa Rais wa Zanzibar katika muda wake wa uongozi, ameweza kufanya yale ambayo hayakuwezwa kufanywa na mtu yoyote toka visiwani hadi bara. Rais Karume anamaliza muda wake, hata hivyo ataendelea kukumbukwa sana kwa hatua yake ya kuwa na maridhiano na CUF.

Sipendi kusema ni maridhinao, bali napenda kusema ni mapatano,kwani sasa ni wakati wa kuelewa na kufahamu siasa za Zenj hazitokai na chuki miongoni mwao bali chuki zilipandikizwa ili kuwezesha chama fulani kushika madalaka. Hivyo sio sahihi kusema ni maridhiano, kwani kwa kusema hivyo bado kutakuwepo na chuki binafsi miongoni mwetu.

Cha msingi ni kusema kuwa zanzibar sasa inaelekea kwenye mapatano ambayo jatajali Wakaazi wa visiwa hivyo zaidi ya itikadi zao za kisiasa. Na ni vema kwa wana visiwani wote kujua hilo na kushiriki kikamilifu katika kura za maoni ili kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Kwa muda mrefu nimekuwa mjumbe wa JF na nimeshiriki kikamilifu katika kutetea siasa za Zenj ikiwa ni pamoja na kuanzisha blog hii. Hta hivyo naona sasa ni muda muufaka wa kupumzika kuogelea siasa na kusubiri maamuzi muafakan ya wananchi wa Visiwani na hatima yetu kisiasa.

Nitaendele kupitia JF kwa kusoma janayojili pasipo kuchangia chochote.


Kwa muda huu napenda kuwajulisha wapenzi wote wa Vituko vya Zenj
kuwa tuwe pamoja katika ujenzi moya wa Zanzibar

10 comments:

Anonymous said...

Are you a Zanzibaris?If not why are so interested in talking about matters from Zanzibar, instead of Tanganyika?

...just curios

Kibunango said...

Ni mtanzania

Anonymous said...

Yah mwenye asili ya Zenj, hilo ndio suali langu...

Shukurani kwa kutupasha habari katika blog hii...

Anonymous said...

nha mimi pia ningependa kuuliza suali ambalo mwanzo lilikosa jibu.

Wewe ni Mzanzibari au ni Mtanganyika?

Kwa sababu ukisema wewe ni Mtanzania bila ya kuwa Mtanganyika ama Mzanzibari basi utakua umechukua tu Uraia.

Shukran

Kibunango said...

Anoy.. wa tarehe 4.
Napenda kurudia tena kusema kwamba mimi ni Mtz, na haijarishi nimehusu sehemu gani, kwani hata pasi yangu ya kusafiria imeandikwa kuwa ni mtz

Anonymous said...

Sasa kaka mzee mbona unakua mgumu kujitambulisha? unaona hata aibu kujivunia asili yako? tunajua kama Utanzania ni utaifa wa mtu lakini kila mtu ana asili yake hata mimi pia ni Mtanzania kwani mkoba wangu umeandikwa Mtazanzia pia, lakini nje ya muungano mimi ni Mzanzibari, sasa na wewe je nje ya Muungano wewe una asili ya wapi? mbona unaona aibu kujinasibu na asili yako.

Anonymous said...

Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulinda umoja wa kitaifa ili wananchi waishi kwa kupendana, kustahamiliana, bila kujali anatoka wapi. kwa hilo Tanzania imefanikiwa kwa kiaji kikubwa na tujivunie kwani angalia nchi nyingi hasa za africa zimekuwa na matatizo kwa sababu ya kujali unatoka wapi au dini yako. Mimi naona huna sababu ya kushindikiza kumuuliza suali kuwa anatoka wapi kama kasema ni Mtazania naona inatosha. kama inahisi hajajibu unavyotaka sijui wewe una ajenda gani kwani hiyo itapelekea kusema wewe ni wa Pemba na wewe wa unguja tutakuwa tunarudi pale pale cha msingi jali maendeleo ya watu na kuboresha umoja.

Anonymous said...

asante sana kaka wa vituko vya zenji kwa blog hii, kwani mimi nimeifuma kupitia blog ya dullonet tz,lakini mbona unatubania hivyo vituko vya ZBR hatuvioni? , ebu tuwekee picha za matukio ya mipasho,midume inayojifanya midada, maana nasikia huko wako wengi sana,je nauliza vipi hali ya kisiasi huko zbr ipo vipi maana huko uchaguzi ukikaribia vituko haviishi

Anonymous said...

Mbona hayo madume yanayojifanya mdada hata huko tanganyika yapo, sio tu Zenji peke yake. imekosa nini zenji?

mrfroasty said...

Na midume mengine pia haijifanyi midada hupenda kufanya mapenzi na midume kama wewe...hadhari inahitajika hapo :D