Tuesday, 9 February 2010

Vyama vingine zaidi vyataka mseto....
Ni baada ya kutoshirikishwa katika mseto wa CCM na CUF

VYAMA 16 vya upinzani visiwani hapa vimekataa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoshirikisha vyama vya CCM na CUF kwa madai kuwa havitaondoa mpasuko wa kisiasa.

Msimamo huo umetolewa jana visiwani hapa na mwenyekiti wa umoja wa vyama 16 vya siasa Zanzibar, Juma Ali Khatib, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Vyama hivyo ni: DP, TADEA, CHADEMA, NCCR Mageuzi, AFP, TLP, SAU, UDP, UPDP, CHAUSTA, UMD, JAHAZI Asila, P.T.P Maendeleo, DEMOCRASIA Makini, NRA na NLD.

Habari zaidi tembelea Mzalendo.net

No comments: