Wednesday 10 March 2010

Huu ni Ujuha au Ujuhaji?


Waznz hatutaki Njia zetu kuitwa majia ya makafiri hawa akina Mkapa na ndugu zake hawana historia zozote znz, kama mumeshindwa kuwa enzi wana vyuoni wetu basi bora muite jina la Bi Kitute Road wazanzibar tutarizika.

Wanao jizalilisha ni ccm-smz sio wazanzibar wote, kuna wana vyuoni wetu na watu wenye historia mzuri Zanzibar na wazanzibar wana zipenda kwa nini hamukuita mumekwenda kuita majina ya wauwaji na walioasha asari za viwete na vizuka. Wakadi kuna historia zetu wenyewe wazanzibar. Au ndio kutawaliwa smz huko? Mungeita barabara ya Sh Amer Tajo,Sh Abdalla Farth,Sitti Binti Sadi, Mwana wa Mwana na Mkama Tume. Hizi ndio historia zetu. Lakini ccm-smz mumeoza kwa watawala wa ki-Tanganyika kama. Kama tulivyo piga kelele iondoshwe historia mpovu isisomeswe maskulini watoto wetu isio wahusu wazanzibar na kuaswa historia yao wazanzibar nah ii ya bara bara iondoswe mara moja.

Zamani utaona watoto wetu wanasomeswa vita vya wahehe na wamanyema vita vya majimaji lakini hatujawahi hata siku moja kusomeswa watoto wetu kuhusu Mkama ndume na Mwana wa Mwana tunasomeswa watoto wetu makabila hata hapa Zanzibar hayapo. Wewe umeona wapi kabila la wahehe hapa? Au wamanema kama sio vishekesho bora kusema Wazaramu wapo Miembeni na kwahani na sasa tuna Wamasai Kiwengwa historia ya badae zenj. Kwa hio wazanzibar tustuke tusikubali kupashikizwa historia zisizo tuhusu.

Hiyo hapo juu ni nukuu toka Mzalendo.net

Baada ya kuisoma imebidi nijiulize kama imeandikwa kutokana na kutojua taratibu za utoaji wa Majina katika barabara, mitaa, na vitongoji au ni ujuhaji mwingi ambao upelekea kwa mhusika kuwa juha! Pichani juu kabisa ni baadhi ya barabara na mitaa ya Mkoa wa Mjini Magharibi.

Kama kawaida mtoa hoja kaficha jina lake, lakini kwa kuwa lengo lake isomwe na kujadiliwa hakuna tatizo katika hilo. Nitajaribu kumfahamisha taratibu za ubadilishaji wa majina ya mitaa, barabara na vitongoji katika Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria ya Manispaa ya Zanzibar ya mwaka 1995 namba 3.

Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar ndio yenye jukumu la kuhudumia na kusimamia barabara, mitaa na chochoro zote zilizopo ndani ya mipaka ya Manispaa hiyo, hii ikiwa ni pamoja na utoaji wa majina kwa barabara na mitaa. Mara ya mwisho ya kufanyika mabadiliko makubwa ya majina katika barabara na mitaa ya Zanzibar ilikuwa ni katika miaka ya tisini ambapo zaidi ya barabara kumi zilipatiwa majina mapya. Kazi hii ilifanya na kamati ya Mipango Mji kabla ya kuthibitisha na Baraza Kuu la Manispaa hiyo.

Vigezo vya ubadilishaji wa majina ya mitaa/barabara hufanywa na Madiwani, na kwa bahati nzuri tokea mwaka 1995 hadi leo Baraza la Manispaa hilo limekuwa na Madiwani toka CCM na CUF. Mtoa hoja katika nukuu hapo juu ametupa lawama kwa CCM - SMZ, napenda ajue kuwa Madiwani hata Madiwani wa CuF walikuwepo. Zaidi ni vema kujua kuwa Madiwani ni wawakilishi wa ngazi ya mwanzo ya wananchi na ndio wapo karibu kabisa na wananchi. Hivyo basi madiliko kama haya huwa kwa namna moja ama nyingine yanabeba maoni ya wananchi wao. Mtoa mada mada sijui anawakilisha maoni ya wadi gani au jimbo? Ni vema akaweka sawa kwenye mada yake ili iweze kufahamika anawawakilisha akina nani!

Ramani iliopo hapo juu pamoja na kutoonyesha barabara zote zilizopo ndani ya mipaka ya Manispaa, pia haionyeshi majina ya mitaa mingi ambayo tayali imeshapewa majina. Hili linaweza kuwa ni tatizo la muundaji/mchoraji wa ramani husika au tazizo la asasi zinazohusika na upasishaji wa ramani kwa matumizi ya jumuiya na watalii.

Hapa chini ni baadhi ya majina ya barabara zilizopo katika Manispaa ya Zanzibar:-

Kutoka Kinazin kwenda Bububu- Aboud Jumbe

Kiembe Samaki hadi Amani- Idrisa A. Wakili

Mnazi mmoja- Airport- Nyerere

Mkunazini hadi Kariakoo - Karume

Maisara - Michenzani kwenda Mlandege- Dr. Salmin Amour


Ule Uchochoro wa Darajani hadi Mlandege- Ali H.Mwinyi

Barabara toka Mazinini kwenda Chukwani - Barabara ya Bakari Jabu



Kwa mtoa hoja bado ana nafasi kubwa ya kuweka kwa majina ambayo anaona yana umuhimu kwa jamii na historia ya Zanzibar. Majina mengi bado yanahitajika na hasa katika Halmashauri ya Mji Magharibi. Ni vema kwake akawasilina na Halmashauri husika na kuona vipi anaweza kuchangia katika kutoa majina mapya.

Mwisho nimeona kuwa kuna utunzaji mbovu sana wa kumbukumbu au kuna njia za makusudi zinazofanyika katika kupotosha majina ya barabara na mitaa.

Mfano mkubwa ni kwa barabara ya Creek. Barabara hii ilishabadilishwa jina zaidi ya miaka ishirini sasa, lakini bado ramani zinazotoka kwa matumizi ya utalii zinatumia jina hilo. Hii ni pamoja na mtaa utakao Darajani hadi Mladenge. Ipo haja kwa vyombo husika kuliona hili.

Kwa upande wa Manispaa ni vema mkarudisha vibao vya majina ya mitaa na barabara, kumekuwepo na tabia ya kuweka vibao hivyo kwa barabara maarufu tu, ni vyema sasa mkaangalia na kuweka vibao katika sehemu ambazo sio maarufu lakini zenye uhumimu sawa na sehemu nyingine maarufu.

3 comments:

Kaziyabure said...

Hoja nzuri Kamanda.
Na barabara ya kutoka Mazizini kuelekea Chukwani inaitwa Bakari Jabu Road!

Kibunango said...

Pouwa, Nitaiongeza
Shukrani kwa picha!

Bennet said...

Sijui ana hisia gani labda ni za kibaguzi na hasa kuwabagua watu kutoka Tanganyika na lazima atakuwa hafurahishwi na huu Muungano, amesahau kwenye historia kwamba Z'bar, Tanga na Mombasa zilikuwa ni milki moja na mpaka leo watu wanaendelea kuoleana sana, sasa ukianza kuwabagua hawa sijui kama tutafika