Saturday, 20 March 2010

Milango ya Zanzibar: Mji Mkongwe


Milango ya Zanzibar ilianza kutumika katika miaka ya 1870 na kupata umaarufu mkubwa hadi sasa.Milango hii ilibuniwa na kuchongwa kufuatana na tamaduni za kihindi na kiarabu.

Katika miaka hiyo ya 18' jumla ya milango 806 ilitengenezwa. Hiki kilikuwa ni kipindi cha Sultan Bargash.Sifa kubwa ya milango hii ni mapambo yake ambayo yalitokana na dhana ya kujikinga na madhara ya kishetani kuingia ndani ya nyumba. Mapambo mengine yaliyomo kwenye milango hiyo ni maua, matawi ya minazi, aya za Koran, jina la mwenye nyumba na mwaka uliotengenezwa mlango huo.

Zaidi baadhi ya milango hiyo imetiwa vyuma umbo la koni nyenye ncha kali ikiwa ni kama silaha ya kujikinga na uvamizi wa Tembo.


Kuna aina mbili za milango hii, moja ni umbo la mstatiri katika sehemu yake ya juu na ya pili ni umbo la nusu duara katika sehemu yake ya juu. Mlango mmoja uchukua muda wa miezi mitatu kutengenezwa na hutumia mbao ngumu aina ya Mninga. Hadi sasa milango hii hutengenezwa kwa kutumia mkono. Hata hivyo katika karakana ya Ofisi ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe, baadhi ya maandalizi ya utengenezaji wa milango hiyo hutumia mashine.


Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe, inastahili kupongezwa kwa kuhakikisha kuwa aina hii ya milango inaendelea kutumika katika Mji Mkongwe. Hii ni kutokana na kuwepo na wimbi kubwa la kung'olewa kwa milango hiyo katika miaka ya 80 kwa lengo la kuuzwa. Adhia kuwepo kwa ubadilishaji wa milango hiyo kutokana na kufanyiwa matengenezo ya nyumba.


Picha ya kwanza juu, gari linaloonekana ndio lilikuwa gari la Prez wa kwanza wa Zanzibar Marehemu A.Karume.

No comments: