Thursday 4 March 2010

Ubaguzi waanza kushika kasi Zanzibar....




Katika tembea tembea mtandaoni, nimekutana na mada hii hapa chini, yenye kila aina ya ubaguzi na chuki za waziwazi, kwa watanzania bara waishio visiwani humu. Hapa chini ni nukuu yake

mkuu wa vitambulisho vya uzanzibar Mohamed Juma Ame anasema waliokosa haki ya kujiandikisha wato hawana sifa za uzanzibar kwa hio sio wazanzibar bona watu wa tanga pangani,mafya na wamasai wa kiwengwa wote wamepata kuandikiswa hiwe nyie tu?

Maskini Mh Shabani Hamis Mloo mawazo yake na busara zake tutazienzi. Aliona mbali aliposema Zanzibar hatuna Serekali tuna kikundi cha wahuni tu. Leo ni Nchi gani ulimwenguni inayo wakataa wananchi wake na kuwanyima haki na kuwakumbatia wageni kwa kuwapa uhalali wa Nchi na usibiticho wa uzawa vyeti vya kuzaliwa na utambulicho wa Zanzibar. Au ndio Msh Karume tulifanya kosa Mh Amertajo alipokula kiapo cha Ushahidi kuwa Father K kazaliwa Mwera ndio kiapo kile kilituzuru wazanzibar wote? Kunahaja ya wazanzibar kujipanga safu na Kenosha mazila ya kila siku kama hatuja pigana coper basi mambo hayawi heat and running mealtime itumike Zanzibar si hivyo Nchi inakwenda na ccm ndio wabeba mashera.

Jina la mtoa mada hii halijabandikwa ila unaweza kutembelea tovuti ya mzalendo kwa maelezo zaidi.

Mada hiyo ni mfululizo wa mada kadhaa zilizoanza kuibuka baada ya mazungumzo ya maridhiano ya Rais Karume na Maalim Seif. Mara baada ya maridhiano hayo, maoni mengi yalielekezwa katika Zanzibar na Muungano wake chini ya kivuli cha utaifa,na kusahau kabisa lengo kuu la maridhiano/mapatano hayo ambayo yalikuwa na lengo la kuijenga Zanzibar moja iliyomeguka kutokana na siasa na kuathiri kwa kiwango kikubwa umoja na undugu wa wananchi wa visiwa hivyo tokea kuingia kwa mfumo wa vyama vingi.

Zanzibar ya leo uchumi wake kwa aslimia 80 unategemea watalii, tokea Zanzibar kufungua milango ya utalii, visiwa hivyo vimeshuhudia uingiaji wa wageni wengi, na wageni hawa wameingia kutokana na kukua kwa utalii na mahitaji ya utalii katika visiwa hivyo, ambayo kwa wakati huo na sasa wakaazi wake hawawezi kukidhi mahitaji ya utalii visiwani humo.

Kumekuwepo na hatua mbali mbali za kuondoa baadhi ya mahitaji ya utalii katika visiwa hivyo kwa nyakati tofauti. Miaka ya mwishoni ya tisini, kulifanyika zoezi kubwa la kuwaondoa wafanyabiashara za vinyago na batiki katika maeneo ya Kiwengwa pasipo mafanikio. Uundoaji wa wafanyabiashara hao ulishindikana kutokana na kuwa ulikuwa hauna maana yoyote zaidi ya chuki na ubinafsi wa baadhi ya viongozi ambao walijiweka nyuma ya pazia la udini.

Zoezi kama hilo lilirudiwa tena kwa wafanyabiashara wa vinyago na batiki katika mitaa ya gizenga na forodhani, na hata liliposhindikana wafanyabiashara hao walihamishiwa katika maeneo ya Maruhubi, na baadae Msikiti Mabluu. Hata hivyo maeneo hayo yalishindikana kufanyika kwa biashara hizo kwani zoezi hilo lilifanyika pasipo kuwepo kwa utafiti wa kina, na baadae ilikuja kujulikana kuwa limetokana na utashi wa baadhi ya watu dhidi ya wafanyabiashara hao.

Shughuli za Utalii hapo visiwani unaweza kuzigawa katika mafungu kadhaa. Kuna vijana ambao wanaitwa mapapasi hawa kazi yao kubwa ni kupokea na kuwazungusha watalii katika mitaa ya mji Mkongwe,kuwatafutia watalii hao sehemu za kumpuzika na kadhalika,Kundi hili linaaminika kujengwa na wazawa. Aidha kuna wakati kundi hili lilitakiwa kujiandikisha kama chombo rasmi ili kijulikane kisheria na kuweza kulipa kodi. Hata hivyo zoezi hili halikuweza kufanikiwa. Kuna kundi la wafanyabiashara ndogo ndogo za vinyago na batiki, kundi hili linaaminika kuundwa na wageni. Na ni kundi ambalo linapata misukosuko isiyo kwisha licha ya nafasi yake kubwa katika utalii visiwani hapo ikiwa ni pamoja na kuingiza mapato yake serikalini.

Mada toka Mzalendo inalalamikia kwa wageni hao kupata haki ya kupiga kura. Sifa mojawapo ya kuweza kupiga kura ni kukaa sehemu moja kwa zaidi ya miaka mitano. Hapana shaka wengi wa wafanyabiashara hawa wana zaidi ya miaka kumi visiwani huo. Hivyo kwa wao kuandikishwa kupiga kura sio suala la kushangaza na kuandikiwa kwa namna hiyo! Zaidi hawa ni watanzania na wana haki ya kwenda sehemu yoyote ya nchi.

4 comments:

mrfroasty said...

Sasa mbona hujadili ni kwanini wazanzibari ambao wamezaliwa visiwani humo na wameishi miaka yote visiwani humo wamekosa vitambulisho hivyo.

Wakati mmasai amepewa?Ni nani asiejua kuwa CCM husafirisha kwa makusudi watanganyika waende kusaidia kupiga kura Zanzibar.

Tunayo hadi majina yao, na si kweli kama wameishi miaka kumi.Wengine wameletwa majuzi tuu, hawana sifa za kupiga kura Zanzibar.

Walitakiwa kupiga kura ya Tanzania tuu, sio Zanzibar.

Kibunango said...

Nafakili una maana ya kupiga kura Tanzania Bara.

Tatizo kubwa kwa baadhi ya wazawa kutoweza kuandikishwa ni kutokana na kushindwa kukamilisha baadhi ya sifa za uandikishwaji. Wengi hawana vyeti vya kuzaliwa na hawana nia ya kuvitafuta ili waweze kuwa na sifa ya kupiga kura.

Hili ni tatizo la mtu binafsi zaidi na sidhani kama inatosha kuuita ni kero!

mrfroasty said...

Acha kutupumbaza kibunango, mimi binafsi yangu nimepata majina 300 kutoka jimbo moja Stone Town.

Watu ni vijana na wote wanavyo vyetu vya kuzaliwa ni wazanzibari, lakini vitambulisho hawajapewa hadi sasa wanazungushwa kwa makusudi.

Sasa sio kama mkwala, lakini wambie jamaa zako wajitayarishe kuekewa ulinzi mkali wananchi wenye hasira wakichukua hatua mikononi mwao...usije sema sijatoa onyo.

Mapanga yetu ya Mapinduzi bado yapo...I mean it.

Sankara said...

Mimi Sihitaji kitambulisho(inanitosha kutambuliwa na hapa mtaani kwangu) kwani ninanaamini vitambulisho ni moja ya hatua ya kubaguanai.hata hiyo kitu inaitwa kupiga kura ni kupumbazana tu!kwaraju ninajulikana,ccm bar ninajulikana,mtendeni ninajulikana,mnazimoja ninajulikana,nikiingia msikitini mweziwa ramadhani sinyimwi tende,mtaani ninaheshimika,nikienda kuangalia mipira mao nina tunashangiria wote, hata dala dala nikipungukiwa nauli ninapanda!sasa hivyo vikaratasi mimi vya nini?utambulisho gani tena huo mimi ninahitaji ili nijijue kama mimi ni mzawa!
Huu upofu wa CUF na CCM umepumbaza jamii ya kizanzibar kwa 99.5% kimawazo.
"...Africa have a longway to go before it reaches realy revolutionary muturity."by che Guevera,the african dream(2000,pg8. the Harvill Press)