Tuesday, 11 May 2010

Wageni wa ajabu! FFU walipotua Mjini Munich na muziki wao!Pichani, Mwenye Miwani Ras makunja kamanda wa Ngoma Africa band aka FFU katikati mwenye kofia nyeupe Afande Chris-B(Mshambuliaji wa solo) wa FFU pembeni ni MR.Reginald Temu mwenyekiti wa chama cha urafiki kati ya wajerumani na watanzania,akiwakaraibisha mjini Munich wageni wa ajabu! FFU wa Ngoma Africa ambao hawana huruma hata kiduchu washambuliapo jukwaani.

Bendi hiyo ya Ngoma Africa ilifanikiwa kuwatia kiwewe washabiki mjini munich usiku
wa 8-05-katika shamra shamra za kusherekea kombe la soka la dunia Afrika Kusini 2010.
Sherehe hizo ziliudhuriwa na wengi na wageni wa heshima, ambao walikuwa ni manaibu mabalozi wa Tanzania na Afrika Kusini nchini Ujerumani. Naibu Balozi wa Tanzania yuko Ujeruamani Mhe.Bw.Ali Siwa na Naibu Balozi wa Afrika Kusini nchini humo Mr.Martin Ngudze.

No comments: