Wednesday 28 July 2010

FFU kupereka mzuka wa dansi FRANKFURT !


Bend maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" aka FFU
wanatarajiwa kutua kwa nguvu zote !katika onyesho kubwa la Afrika & Karibik Festival,
litakalofanyika katika Viwanja vya Robestock Park, Frankfurt,Ujerumani siku ya Jumamosi
07-08-2010 maelfu ya washabiki wa mziki nchini ujerumani wanaisubiri bendi hiyo kwa hamu kubwa...
kutokana na mdundo wake unaochezeka.

Habari zinatonya kuwa bendi hiyo pia itatingisha jukwaa katika onyesho lingine kubwa
la Festival mjini keiserslautern,Ujerumani siku ya Jumapili 8-08-2010 ambako katika kila
hali washabiki wapo tayari kwenda sambamba na gwaride la FFU wa Ngoma Africa band.
usikose kujipa raha mwenyewe kwa kuwasikiliza hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica

No comments: