Tuesday, 3 August 2010

Hamad Masauni aibuka kidedea Kikwajuni


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM, Hamad Masauni Yusuf, ameshinda katika kura za kugombea nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kikwajuni kwa kura 990.

Hamad ameweza kumshinda Naib Katibu Mkuu wa CCM Saleh Ramadhani Feruzi ambae aliweza kupata kura 155 na kushika nafasi ya tatu chini ya Ahmed Mohamed aliyepata kura 511.

No comments: