Monday, 12 September 2011

Salam za Rambirambi kutoka kwa Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)

Watanzania tunaoishi ujerumani tumesikitishwa sana na habari mbaya ya ajali ya meli iliyotokea 10.09.11 katika bahari ya hindi katikati ya visiwa vya Pemba na Unguja nchini Tanzania. Ajali hii ni pigo na msiba mkubwa kwa Taifa letu. Salam za rambirambi ziwafikie Familia za wafiwa, Viongozi wa Tanzania, na watanzania wote kwa ujumla.

Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) kwa masikitiko makubwa tunaungana na wanafamilia, na taifa zima katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa vyombo mbali mbali kwa jitihada zake za kuokoa maisha na kusaidia kwa namna moja au nyingine katka janga hili kubwa kwa Taifa
Tunaomba kwa mwenyezimungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi amen

-- kny ya UTU

Mfundo Peter Mfundo
Mwenyekiti

No comments: