Sunday, 9 October 2011

Nyerere Day 2011 in Washington DC

Maadhimisho ya nne ya kuenzi maisha na kazi za Mwl Julius K. Nyerere yatafanyika Oktoba 15, 2011 hapa Washington DC. Mmoja wa waasisi wa Julius Nyerere Comemoration Bwn Rick Tingling akielezea maandalizi ya siku hiyo katika video hapa chini
http://www.youtube.com/watch?v=dfp2o_kTmyw

NYOTE MNAKARIBISHWA

Itafanyika
Howard University Basement Auditorium
725, 2225 Georgia Ave, NW, Washington, DC 20059
FROM 3PM-6PM

MAELEKEZO KUELEKEA Howard University Hospital Basement Auditorium:
1.Ingilia mlango wa mbele wa Hospitali unaotazamana na Georgia Avenue.
2.Pita kwenye dawati la maelezo kwa utambulisho
3.Endelea mbele mpaka kwenye "lift" zilizo kama yadi 50 toka dawati la mapokezi.
4.Chukua "lift" / elevator kuelekea sakafu ya chini (basement).
5.Elekea upande wa kulia ukifuata alama zinazoelekeza ulipo ukumbi.


NOTE: Mabadiliko pekee niliyojulishwa ni kuwa Balozi Mwanaidi Maajar hataweza kuhudhuria kwa kuwa atakuwa nje ya mji.

No comments: