Wednesday, 18 July 2012

Meli Kwa Jina la Skagit Imezama Karibu na Chumbe

Ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Unguja, ikiwa na abiria 200. Kazi za uokoji zimeshaanza.

Boat za Sea Star na Kilimanjaro zimekwenda kwenye eneo la tukio kwa ajili ya uokoaji.. Habari zinasema kuwa miili ya abiria imeanza kuonekana ikielea. Hali ya bahari ina upepo mwingi kwa sasa.

Aidha kutokana na hali mbaya ya hewa meli moja imeshindwa kufika katika eneo la tukio na imerudi bandarini.

Mamia ya watu wapo bandarini Malindi wakiendelea kusubiri watakao okolewa.


Baadhi ya abiria waliookolewa

1 comment:

Anonymous said...

Hii tena imekua mchezo kila mara watu kufa kama kuku, Serikali lazima ichukue hatua kali sana kwa wenye hizi meli si kuacha wanaua watu hovyo, Wanafikiria pesa kuliko roho za watu huu ni uaji umekua si ubinadamu na seriakali inachangia kwa haya yote yanayotokea inakula rushwa kuuwa wanachi wake huu ni upumbavu mkubwa sana.