Sunday 29 September 2013

Wanasiasa...

Sunday 1 September 2013

Ni Sawa kabisa kutimuliwa kwa Mansoor !


Hakuna Jipya au la kushangaza kwa kutimuana mwanachama katika chama cha Kisiasa .

Mtindo wa mwana siasa wa chama hiki au kile kufukuzwa chamani si jambo jipya duniani.
Si Jipya wala si haramu,kwa sababu ni jambo la kawaida . Si chama cha CCM, ndicho kinachofukuza watu chamani . CUF - wamemfukuza Rashid Hamadi na wengineo . CHADEMA - kimewafukuza mamia ya wanachama waliopinga siasa potoshi za kikabila .

George Galaway , wa Uingereza , alifukuzwa katika chama Labour. ANC - wamefukuza Malema Kagema - amewafukuza na hata kuwafunga waliompinga.Museveni,nae amefanya hayo hayo na zaidi ya hayo na vipo vyama vingi na wengi wengineo duniani.

Kwa nini hii leo iwe kero kwa sababu CCM imemtimua Mansoor?

Huu ndio ujuha wa akili za wapinzani.

Uwanachama na kuigia katika chama maana yake ni kuamini -SERA NA ITIKADI ZA CHAMA.
Unapo kwenda kinyume na SERA NA ITIKADI ZA CHAMA ,ni sawa na kujitowa katika chama.Hilo si jambo geni kwa mwenye akili. Ikiwa mtu hakubaliani na sera za chama pana mambo mawili:

Ama kungojea kufukuzwa kama vile alivyofanya Mansoor au kujitoa mwenyewe kwa hiyari ikiwa mtu ni mstaarabu.
Baadhi ya watu wanataka kumvalisha Mansoor ,kilemba cha ukoka katika michakato kwenye masuala ya kile kiitwacho "Masilahi ya Chama" na "Masilahi nchi " - maanenohaya kwa kweli ni political jagons/rhetorics za kipotoshi za kisiasa zinazotumiwa na vipofu wengi wa siasa za CUF ambao wanataka kubabaisha UMMA wa wananchi .

Wanao piga debe la CUF utawasikia wakisema "Tunapigania masilahi ya nchi sio masilahi ya chama ".

Kwani masilahi ya chama na itikadi zake zinapiganiwa kwa sababu ya mawingu na upepo au kwa sababu uboreshaji wa hali ya maisha ya wananchi katika nchi ya Zanzibar?

Kwani chama kisiasa kinapopigania kushika khatamu za utawala,kwa mujibu wa "Sera na Itikadi za Chama " hawasemi kua "sera zao na Itikadi zao ikiwa za Kiliberali au za kijamaa ndizo sambamba na masilahi na mahitaji ya nchi ?

Sasa hawa wapi madebe matupu kwa nini wanataka kutofautisha "MASILAHI YA CHAMA NA MASILAHI YA NCHI "?.

Kuhusu haki ya Kikatiba ya nchi kuwa ni juu na ya nguvu zaidi kuliko haki za chama .

Katiba ya nchi inampa kila mwananchi haki sawa ya kujitamka,kutowa fikira zake,na kuamini akitakacho bila ya woga au wasi wasi na vitisho. Na ndio maana kila mwananchi anatumia uhuru huo na haki hizo za kuchaguwa chama au hata Dini aipendayo kwa mujibu wa imani yake .

Kwa mfano.
Mwananchi anapo kubaliana na kuamini Dini ya Uisilamu - mtu huyo hawezi kamwe kuubiri ukristo msikitini, akifanya hivyo bila ya shaka ATATIMILIWA BILA YA HURUMA .

Mwananchi yeyote yule anapojiunga kwa mfano kwenye chama CUF - haitawezekana kamwe awe anapita pita kuubiri mambo ya siasa za Chadema seuze za CCM -mwanachama huyo hapana shaka atatimuliwa kama vile walivyotimiliwa akina Rashid Hamadi na wenzake wengi.Viongozi wa CUF walifanya hivyo bila ya aibu na kutowa sababu za kama wao ni watume wa mambo ya kisiasa Kijiweni.

Kwa nini liwe kubwa kwa kufukuzwa kwa Mansoor ?
Kwa nini Mansoor ,asitimuliwe wakati hafuati miongozo na sera za chama cha CCM.Wananchi wa Zanzibar mnapenda sana kudangwa na kujidanganya -ukweli mnauogopa na mnachaguwa uwongo kuufanya ndio Ukweli.

Wengine wanasema Mansoor ,hastahiki kufukuzwa kwa sababu uzaliwa wake na Yusuf Himidi.

Wengine wanasema amefukuzwa kwa sababu mama yake ni mwarabu. Kufukuzwa kwake ni kinyume na katiba ya nchi.

Wapinzani wanaropokwa maneno mengi ama kutokana na ujinga wao wa kisiasa au chuki zao dhidi ya CCM.

Sababu zote tatu ni potoshi na ni kasuma za wenda wazimu wenye ukosefu wa ukomavu wa kisiasa .

Tokea lini haki ya kuchagua na kujitamka kurithiwa kutoka kwa bibi ?
Itakuwaje Kukubaliwa au kukataliwa uwanachama iwe kwa sababu za uasili wa wazazi wa mwananchi? Imekhusu nini kuingiza Katiba ya Nchi na suala uwanachama katika chama cha siasa?.

Katiba ya nchi yeyote kwenye nchi za ustaarabu wa haki za Binaadam haiwezi kulazimisha chama chochote kuingiza au kumtowa mwananchi chamani . Kuingia au kutoka katika chama ni uhuru wa mtu. Kuchaguwa na kuomba kuchaguliwa VIVYO HIVYO ni haki ya kila mwananchi.

Chama chochote cha Kisiasa ni sovereign kujiamuliya kuhusu uwanachama kwa misingi ya sheria na kanuni zake kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kila chama kina haki ya kumkubali au kumkatalia uwanchama mtu yeyote ,ikiwa baba yake alikuwa mwana mapinduzi baada ya kuuwa watu au ikiwa baba yake alikuwa shekhe au shoga hiyo haikhusiani na lolote.Ikiwa anaetaka uwanachama haaminiki katika imani na itikadi au ni mweda wazimu kwa nini apewe uwanachama ?

Kikawaida mtu mstaarabu anatafuta uwanachama kwa mujibu wa Itikadi zake ,Mansoor ameingizwa CCM kilazima na kwa sababu zake za kibinafsi sio kwa Itikadi za kisiasa.Yeye kunako mfaa ni CUF NA WENZAKE .

Tokea lini ukamuona Mkoministi kuingia katika chama cha wanaopenda Uleberali - mambo ya haki za Ushoga na Usagaji ?

Kila mwananchi ambae anapenda siasa za Kiliberali za kama za CUF -anataka nini katika CCM wakati chama hiki ni cha siasa za Ujamaa ? Tokea lini Mkiristo kutaka kusaliya Msikitini ? Kwa hivyo Mansoor ,lake ni kuenda kule kwa anaosikilizana kwa yote
na hasa kisiasa- si kwengine ni kule kule CUF. TATIZO LIKO WAPI ?

Tutahadhari kuigizwa katika Ujinga na Jazba ,za kwamba kila asiyetaka siasa ya MAMLAKA KAMILI NI MSALITI NA HAPAENDELEI "masilahi ya nchi " - sasa kwa lugha HIYO HIYO ya Ma-CUF sasa ule uhuru na haki kwa wote Kikatiba haki ya Kujitamka,Kufikiri na Kuchagua haija tuhusu "sisi tusio taka kuuvunja Muungano.?".

HAKI HIZO HATUNAZO KWA SABABU HATUKUBALIANI NA SIASA POTOSHI ZA CUF - KWA HIVYO NI WASALITI.
Tunacho kijuwa sisi ni kwamba ishara za Usaliti zipo kwa CUF ,kwa sababu ya UADUI WAO WA KUTAKA KUUVUNJA UNDUGU WETU WA JADI BAINA YA ZANZIBAR NA TANGANYIKA = MUUNGANO WA TANZINIA .

MUUNGANO OYEE IKIWA KWA SERIKALI MBILI AU TATU NA KUELEKEA KWA SERIKALI MOJA.

MUUNGANO OYEE !



Ali Mtsashiwa