Tuesday, 14 January 2014

Balozi aibiwa simu Ikulu Zanzibar....


Balozi mmoja anayeiwakilisha nchi yake hapa Tanzania, jana jioni ameibiwa simu inayokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya mili 1.5.

Tukio hilo limetokea jana kwenye chakula cha pamoja cha viongozi wa kitaifa na wageni wa kimataifa hasa mabalozi iliyofanyika Ikulu mjini zanzibar.

Wageni wote waliokuwepo ni wa hadhi ya juu akiwemo raisi Kikwete na rais Shein na wengne ni wafanyakazi wa Ikulu tu waliokuwa wahudumu.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa mjini magaribi ameeleza kuwa balozi huyo anayesadikiwa ni wa kutoka Sweden atakuwa amesahau tu alipoiweka simu yake kwa kuwa wageni wote waliokuwepo hakuna anayeweza kuiba simu.

Jina na nchi anayotoka balozi huyo limefichwa kulinda hadhi na mahusiano ya nchi hzo mbili.

Source: Tanzania Daima

No comments: