Thursday, 10 July 2014

Wachapwa Bakora Kwa Kula Mchana - PembaChake Chake. Pemba
Vijana wawili kama wanavyooneka kwenye picha hapo juu, walijikuta kwenye wakati mgumu, baada ya kuchapwa bakora ikiwa ni adhabu kwao kwa kula hadharani mchana.

Ikumbukwe kuwa hairuhusiwi kula hadharani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Adhabu ya kawaida kwa anayekula ovyo mchana ni kufungwa kwa mwaka mmoja gerezani.

Hata hivyo kumekuwepo na ongezeko la watu wanaojilia ovyo majiani, kiasi kwamba sasa wanachapwa viboko kabla ya kukabidhiwa kwa vyombo husika kwa adhabu zaidi.