Monday, 26 January 2015

Mawaziri wa Afya Zanzibar na wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Wakutana na Watanzania - Ujerumani


Mhe. Seif Rashid, Waziri wa Afya Zanzibar.


Mhe. Rashid Seif Suleiman, Waziri wa Afya Tanzania.


Baadhi ya Watanzania (FFU-Ujerumani)katika picha ya pamoja na Mhe. Rashid Seif Suleiman


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Seif Rashid na Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe. Rashid Seif Suleiman, Siku ya jumapili 25 Januari 2015, walikutana na kuongea na baadhi ya Watanzania waishio nchini Ujerumani katika Hoteli ya Martim, mjini Berlin.

Mawaziri hao kwa pamoja waliongozana na balozi Tanzania nchini Ujerumani mheshimiwa Bw.Philip Malmo,katika mkutano huo Mawaziri hao wote walielezea jinsi wizara zao zinavyofanya kazi kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafakia walio wengi na pia kuhakikisha siku za usoni kila mtanzania atanufahika na huduma hizo kwa kutumia bima ya afya bila kujali tofouti za uwezo wa vipato vyao.

Watanzania waishio ujerumani wamefarajika sana na mkutano huo, pia Mawaziri wamewataka Watanzania waishio ughaibuni kuchangia kuwekeza katika sekta ya huduma ya afya hata ikiwa ni sekta binafsi,

Mawaziri hao wamesema milango ya wizara zao hipo wazi kwa watanzania wanaotaka ushauri,ushirikiano au kuwekeza katika sekta hizo.Source: Msema Kweli- Ujerumani

No comments: