Tuesday 27 January 2015

Zitto Ruyangwa Kabwe, Ndie Kinara Katika Twitter Tanzania




Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto R. Kabwe 38 ndie mtanzania na mwanasiasa mwenye wapenzi wengi zaidi katika mtandao wa Twitter nchini Tanzania. Zitto ana zaidi ya wapenzi/wafuatialiaji 220K, hivyo kumweka katika nafasi ya kwanza kwa nchi ya Tanzania kwa mjibu wa mtandao wa Socialbakers.

Matumizi ya mtandao wa Twitter katika Tanzania umewaweka kando wanasiasa, ukimwondoa Mhe. Zitto ambae pia ni mwanasiasa toka Chama cha Upinzani. Wengi wenye wapenzi wengi katika Tanzania ni Wasanii kwenye fani za Muziki na Vichekesho. Hii ni tofauti kigodo na baadhi ya nchi zingine katika Afrika. Kwa mfano Afrika ya Magharibi, Wachezaji wa mpira wa miguu ndio wenye wapenzi wengi kama vile Didier Drogba wa Cote d'Ivoire mwenye wapenzi 520K, Mali ni Frederic Kanoute mwenye wafuatiliaji 213K na Togo, Emmanuel Adebayor ndie kinara akiwa na jumla ya wafuatiliaji 137K.

Kwa Afrika ya Mashariki,jirani zetu Kenya, Rais Uhuru Kenyatta ndie mwenye wapenzi wengi zaidi nchini humo kwa idadi ya 716K, hali Uganda nafasi ya juu ikishikwa na mfanyabiashara Ashish J. Thakkar mwenye wafuatiliaji 720K, huku Rwanda nafasi ya kwanza ikienda kwa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame kwa kuwa na wafuatiliaji 786K.

Tukirudi hapa Tanzania Wasanii ndio wanao wafuatiliaji wengi, kama vile Masanja Mkandamizaji 181K, Millardayo 190K,Ambwene AY 164K, Diamond Platnumz 154K, Jokate Mwegelo 160K, MwanaFa 145K.

Mfanyabiashara mwenye wapenzi wengi hapa nyumbani ni Reginald Mengi akiwa na wafuatiliaji 130K.

Kwa upande wa Zanzibar, Zantel ndio yenye wafuatiliaji wengi wakiwa ni 7K

No comments: