Tuesday 4 October 2016

Ashauri Mahari Ilipiwe Kodi ...



MWALIMU wa somo la biashara katika skuli ya sekondari ya Chasasa Wete Pemba Ali Hamad Nondo, amezishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ na Bodi ya Mapato Zanzibar ‘ZRB’ kuchukua kiwango cha fedha (VAT) kwenye vyeti vya ndoa, ikiwa ni njia nyengine ya kukuza pato la taifa.

Alisema hata mahari nayo yamekuwa yakipanda siku hadi siku, na wakati wa kufungishwa kwa sunna hiyo, hutolewa cheti cha ndoa baada ya maharia kulipwa, hivyo ni yema kukawa na kiwango cha fedha kinachoingia serikalini.

Mwalimu huyo, ametoa ushauri huo alipokuwa akichangia mada kadhaa kwenye semina ya siku moja ya kuelezea umuhimu wa kulipa kodi, kwa wanafunzi na waalimu wa skuli hiyo.

Alisema kama bado TRA na ZRB hawachukua ‘VAT’ kwenye cheti cha ndo, wakati umefika sasa kufanya hivyo, maana kwenye taratibu hizo huwepo kwa cheti cha ndoa kutoka mamlaka za kiserikali.

“Mimi nauliza kwenye cheti cha ndoa kuna VAT, kama jawabu hakuna sasa anzisheni hiyo, ili mfuko wa serikali ukuwe, maana nayo mahari yanapanda kila siku’’,alishauri.

Akijubu hoja hiyo, Afisa Uhusiano wa Bodi ya Mapato Zanzibar ‘ZRB’ Khamis Makame Mohamed, alisema kwa sasa wao hawakusanyi hata shilingi moja kwenye cheti cha ndoa, ili kama jamii ikiridhia ni jambo jema.

“Hili ni jambo jema, sisi tutalichukua na kulifikisha kwa wenzetu, lakini kwa sasa pamoja na mahari kuonekana kupanda juu, lakini hatuna kodi, maana kwanza ni jambo la kiimani linataka ufafanuzi wa kina”,alieleza.

Nae Afisa Elimu kwa walipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ofisi ya Zanzibar, Saleh Haji Pandu, alisema kwa sasa mamlaka hiyo, inakusanya ushuru wa forodha na kodi ya mapato pekee na wala sio kwenye cheti cha ndoa.

Mapema akizungumza kwenye semina hiyo, Afis huyo wa elimu kwa walipa kodi, aliwataka wanafunzi na waalimu hao kuwa wa mwanzo kuwadai risiti za bidhaa wafanya biashara mara wapato huduma.

“Nyinyi muwe mabalozi kwa wafanyabiashara kwamba mkishanunua bidhaa msisite kuwataka wawape risiti, maana kama hakutoa huyo ni ehemu ya kukwep kuliopa kodi.

Wakichangia mada kadhaa kwenye semina hiyo, washiriki hao walipendekeza iwepo taasisi moja pekee ya kukusanya kodi ili kuwapungizi usumbufu wafanyabiashara.

Mwanafunzi Yasseir Hamad Ali, alisema itakuwa jambo la busara kama kutakuwa na chombo kimoja cha kukusanya kodi ili iwarahisishie wanaopaswa kulipa kodi moja kwa moja.

Semina kama hiyo juzi walifanyiwa waandishi wa habari na wafanyabiashara kwa lengo la kukuza uwelewa wa ulipaji kodi kupitia TRA na ZRB.
………………………………..

Sunday 14 August 2016

TANZIA : Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia



Rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia leo hii.

Marehemu alizaliwa tarehe 14.06.1920.

Marehemu alikuwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar tokea mwaka 1972 hadi 1984.

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi.

Sunday 26 June 2016

Mv Happy yazama karibu na Kisiwa cha Chumbe....



Meli ya mizigo iitwayo Happy ikitokea Dar es salaam kwenda Zanzibar imezama eneo la Chumbe, Unguja.

Taarifa zimedai kwamba Meli hiyo ilianza kuzama saa 10 alfajiri baada ya kuingiza maji ndani na kukosekana kwa vifaa kama motor ya kutolea maji hayo kufikia saa 1 asubuhi hii Meli hiyo ilizama kabisa ndani ya maji.


Meli hiyo ilikuwa imebeba Dengu gunia 450 pamoja na Mbao zaidi ya 1000 huku wafanyakazi sita waliokuwa ndani ya Meli hiyo wakiokolewa.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ni meli ya mizigo mitupu na mabaharia mpaka sasa imeripotiwa kwamba wote ni wazima.


Source: Jamiiforums

Wednesday 1 June 2016

Zanzibar's pioneering pension scheme.....



Tanzania’s semi-autonomous archipelago of Zanzibar has introduced a pension scheme for all citizens aged 70 and over.

It is the first fully funded state pension in East Africa.

Each pensioner will be entitled to 20,000 Tanzanian shillings ($9, £6) a month.

Campaigners have welcomed the move and say it will lead to a huge improvement, not just in the lives of the elderly - considered to be among the poorest in society - but for the rest of the country as well.

Source:

BBC Africa.

Tuesday 31 May 2016

Ulinzi Mkali Leo Kuelekea Polisi Ziwani...



Ni baada ya Maalim Seif kutakiwa kufika Polisi kwa kuhojiwa.

Wednesday 18 May 2016

Monday 16 May 2016

Maalim Seif Awasha Moto Upya Zanzibar




Maalim Seif Awasha Moto Upya Zanzibar.....Awataka Wananchi Wasilipe Kodi na Waandae Siku ya Mgomo.


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amewasha moto upya visiwani Zanzibar kwa kuwahimiza wananchi kufanya vitendo vinavyoonyesha kuikataa serikali inyoongozwa na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein


Maalim aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na watendaji na viongozi wa CUF kutoka Wilaya ya Micheweni katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tano hapa.

‘Tukikazana, serikali hii itaondoka, ikiwa mnangoja Maalim Seif au Marekani kuiondoa, kwa sheria ya kimataifa haitawezekana kwani Marekani haiwezi kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar,” aliongeza Maalim Seif, ambaye alijitoa kwenye uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika Machi 20, mwaka huu na Dk Ali Mohamed Shein kuibuka mshindi.

Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ulifanyika baada ya Tume ya Uchaguzi ya huko kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Hata hivyo, Maalim Seif alisema Serikali ya CCM imeanza kutikisika kutokana na vikwazo vinavyoendelea kuwekwa na wahisani pamoja na hatua ya chama chake CUF kutowatambua viongozi wake pamoja na serikali.

“CCM wajue wamekalia kuti kavu, siku yoyote wataanguka...tufanye kazi mpaka haki yetu tuhakikishe imerudi na wenzetu hawana safari ya kudumu,” alisema Maalim Seif.

Aidha, alisema Mataifa ya Ulaya zikiwamo Marekani, Uingereza, Norway pamoja na Umoja wa Ulaya, yameanza kuchukua hatua za kuinyima misaada ya maendeleo Tanzania ikiwamo Zanzibar kutokana na mgogoro wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

Alisema wahisani hao pamoja na Shirika la Changamoto la Milenia (MCC) wamesema hawatotoa msaada mpaka suala la uchaguzi la Zanzibar likae sawa na kupatiwa muafaka wake.

Maalim Seif aliwataka wanachama wake kuonyesha kwa vitendo vya kweli vya kutoitambua serikali ikiwamo kukataa kulipishwa kodi za ovyo vyo pamoja na kujitenga na viongozi wa serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Mfano tunaweza kuamua siku flani kuanzia saa sita, tunasimamisha vyombo vyote vya usafiri na siku nyingine tunaamua kupiga honi Zanzibar nzima kuonyesha hatuitaki serikali ya CCM" Alisema Maalim Seif huku akishangiliwa na umati uliofurika katika ofisi za chama hicho.

"Wanasema ukitaka kumshinda adui unampiga akiwa dhaifu na udhaifu wao hawana fedha, na ili kuwadhibiti ni kuwanyima fedha na kuwachokoza kwa kuwaita majina mabaya kama dikteta, Nduli," alisema.

Kuhusu suala la wakulima kuuzia serikali karafuu au kutoiuzia, alisema wananchi wenyewe ndiyo watakaoamua, lakini lengo la CUF ni kuona Serikali ya CCM inashindwa kuongoza Zanzibar kabla ya kumalizika miaka mitano.

Kwa mujibu wa Maalim Seif, tayari hali mbaya ya kiuchumi imeanza kujitokeza Zanzibar kutokana na bajeti ya mwaka huu kupoteza miradi mingi ya maendeleo kwa ufinyu wa fedha.

Kuhusu vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu, Maalim Seif alisema tayari yupo mwanasheria mzalendo ambaye ameanza kukusanya vielelezo mbalimbali kabla ya kufungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa dhidi ya viongozi wenye dhamana ya kusimamia vyombo vya ulinzi na usalama wa raia.

Alisema tayari Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Muungano, wamepewa notisi ya kuarifiwa kufunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa kutokana na vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu uliofanyika Zanzibar.

Alisema kwa sasa wanasheria wanapitia sheria kwa umakini za kuanzishwa kwa mahakama hiyo ya kimataifa ili kuangalia uwezekano wa serikali ya Zanzibar kufunguliwa mashtaka katika mahakama hiyo.

Wakati wa ziara hiyo, Maalim Seif alipata wakati mgumu kutokana na barabara kufungwa na wafuasi wake wakimtaka atoe kauli juu ya hali ya kisiasa ya Zanzibar.

Thursday 31 March 2016

Nyumba inauzwa Maungani - Zanzibar



Nyumba inauzwa ipo Maungani, ina vyumba 4 na vyoo 3. ni ya kisasa na ipo katika hali nzuri. Pia ipo ndani ya uzio.

Kuna banda la mtumishi au housegirl ambalo lina chumba na choo jiko na stoo.

Bei ni shs 95,000,000

Kwa maelezo zaidi au kuiona piga simu namba 0777275551. ulizia nd. Khalid

Monday 21 March 2016

Dkt Shein Ashinda Uchaguzi Zanzibar



Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar nd.Jecha Salum Jecha amemtangaza Dkt Ali Mohamed Shein kuwa Rais Mteule wa Zanzibar kwa kura 299,982 sawa na 91.04% ya kura zote zilizopigwa.

Kwa ushindi huo anayefuata kwa matokeo hayo ni Hamad Rashid ambaye amepata kura 9734 sawa na 3%.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ametangaza matokeo hayo kama ifuatavyo.

1 Khamis Iddi Lila ACT-Wazalendo kura 1225 sawa na 0.4%

2 Juma Ali Khatib ADA-TADEA kura1525 sawa na 0.5%

3 Hamad Rashid Mohamed ADC kura 9734 sawa na 3%

4 Said Soud Said AFP kura 1303 sawa na 0.4%

5 Ali Khatib Ali CCK kura 1980 sawa na 0.6/

6 Ali Mohamed Shein CCM kura 299,982 sawa na 91.04%

7 Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA kura 495 sawa na 0.2%

8 Seif Sharif Hamad CUF kura 676 sawa na 1.9%

9 Taibu Mussa Juma DM kura 210 sawa na 0.1%

10 Abdalla Kombo Khamis DP kura 512 sawa na 0.2%

11 Kassim Bakar Aly JAHAZI kura 1470 sawa na 0.4%

12 Seif Ali Iddi NRA kura 266 sawa na 0.1%

13.Issa Mohammed Zonga SAU kura 2018 sawa na 0.6%

14 Hafidh Hassan Suleiman TLP kura 1499 0.5%

Aidha Mwenyekiti wa Tume hiyo amesisitiza kwamba wagombea wote 14 walishiriki uchaguzi huo na hakuna aliyejitoa kama vyama vilivyotangaza kwa sababu hawakufuata sheria ya uchaguzi iliyowataka kujitoa siku ya kutangazwa kushiriki uchaguzi ambayo ilikuwa ni tarehe 06.09 2015.

Saturday 5 March 2016

Zanzibar Poll Will Be Successful - Samia



The government remains committed in ensuring that the elections in Zanzibar are conducted and concluded well later this month.

Vice-President, Ms Samia Suluhu Hassan made the remarks yesterday in Dar es Salaam when officiating at the 9th Inter-Parliamentary Relations Seminar known as Nanyuki IX Series.

"During the forthcoming Zanzibar elections citizens should comply with all set election laws, guidelines and principles," said the VP. She praised the selection of the theme "Compliance with African Union and Sub-Regional Blocs' Election Benchmarks: the case of the EAC" as being timely.

Through the seminar, the East African Legislative Assembly (EALA) has taken a strong resolve to appropriately remind governments, electoral management bodies and all stakeholders engaged in electoral process to conduct polls in transparent manner while upholding the declaration of results.

"The issue of credible election in Africa and the attendant sub-regional bodies and the smooth transfer of power is one that cannot and must never be wished away.

Source:Daily News

Sunday 7 February 2016

Mazombi Zanzibar....


Kumekuwepo na watu wanaojifunika soksi kichwani ambao kwa muda sasa wamekuwa wakipiga watu kwa kutumia silaha za aina mbalimbali katika mji wa Unguja. Watu hao wanajulikana kama Mazombi.

Kupitia kwa Kamishna wa Polisi Zanzibar, Jeshi la Polisini Visiwani humo linasema, halina taarifa za kuwepo kwa Mazombi...

Habari zaidi ingia hapa