Monday, 21 March 2016

Dkt Shein Ashinda Uchaguzi ZanzibarMwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar nd.Jecha Salum Jecha amemtangaza Dkt Ali Mohamed Shein kuwa Rais Mteule wa Zanzibar kwa kura 299,982 sawa na 91.04% ya kura zote zilizopigwa.

Kwa ushindi huo anayefuata kwa matokeo hayo ni Hamad Rashid ambaye amepata kura 9734 sawa na 3%.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ametangaza matokeo hayo kama ifuatavyo.

1 Khamis Iddi Lila ACT-Wazalendo kura 1225 sawa na 0.4%

2 Juma Ali Khatib ADA-TADEA kura1525 sawa na 0.5%

3 Hamad Rashid Mohamed ADC kura 9734 sawa na 3%

4 Said Soud Said AFP kura 1303 sawa na 0.4%

5 Ali Khatib Ali CCK kura 1980 sawa na 0.6/

6 Ali Mohamed Shein CCM kura 299,982 sawa na 91.04%

7 Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA kura 495 sawa na 0.2%

8 Seif Sharif Hamad CUF kura 676 sawa na 1.9%

9 Taibu Mussa Juma DM kura 210 sawa na 0.1%

10 Abdalla Kombo Khamis DP kura 512 sawa na 0.2%

11 Kassim Bakar Aly JAHAZI kura 1470 sawa na 0.4%

12 Seif Ali Iddi NRA kura 266 sawa na 0.1%

13.Issa Mohammed Zonga SAU kura 2018 sawa na 0.6%

14 Hafidh Hassan Suleiman TLP kura 1499 0.5%

Aidha Mwenyekiti wa Tume hiyo amesisitiza kwamba wagombea wote 14 walishiriki uchaguzi huo na hakuna aliyejitoa kama vyama vilivyotangaza kwa sababu hawakufuata sheria ya uchaguzi iliyowataka kujitoa siku ya kutangazwa kushiriki uchaguzi ambayo ilikuwa ni tarehe 06.09 2015.

No comments: