Monday, 19 February 2018

Kiringo Mikononi Mwa Polisi....Jeshi la POLISI MKOA WA MJINI MAGHRIB linamshikilia Mtumishi wa bodi ya mapato Tanzania (TRA)  kwa tuhuma za kumlawiti Kijana wa kiume mwenye Umri wa miaka 13. Mtuhumiwa huyo anatambulikana kwa jina la KIRINGO  amekamatwa leo na yupo chini ya ulinzi wa jeshi hilo.. 

Aidha KAMANDA WA POLISI MKOA WA MJINI MAGHARIB HASSAN NASSIR ALI amethibitishwa kukamatwa kwa mtuhumiaa huyo katika maeneo ya uwanja wa ndege Zanzibar alipokuwa akisafiri

KIRINGO aliwahi kushutumiwa kwa matukio tofauti ya namna kama hiyo kabla ya tukio hili, wananchi wamekuwa wakipiga kelele kwa kuharibiwa vijana wao na mtuhumiwa huyu. 

Ikumbukwe katika ziara ya mkuu wa mkoa wa mjiji Magharibi Muheshimiwa Ayoub Muhammed Mahmoud alipokuwa akisikiliza kero za wananchi wa mkoa wake, wananchi walimlalamikia kuwa Kiringo anaharibu vijana wengi lakin polisi bado hawajamkamata, na ndipo Mkuu wa Mkoa wa mjini alipomtaka kamanda wa polisi Mkoa wa mjini ajibu na akasema kuwa wao kama polisi wamesikia sana malalamiko hayo,lakin bado hawajapata ushahidi wa matukio hayo. Na akasema pindipo watakapopata ushahidi basi watamshikilia na kumfungulia mashtaka.

Baada ya ziara hiyo ya Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi ndio imeamsha hisia za jeshi la polisi kumfatilia na kumchunguza mtu huyo.Source: Karafuu24

No comments: