Sunday, 14 August 2016

TANZIA : Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia



Rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia leo hii.

Marehemu alizaliwa tarehe 14.06.1920.

Marehemu alikuwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar tokea mwaka 1972 hadi 1984.

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi.

Sunday, 26 June 2016

Mv Happy yazama karibu na Kisiwa cha Chumbe....



Meli ya mizigo iitwayo Happy ikitokea Dar es salaam kwenda Zanzibar imezama eneo la Chumbe, Unguja.

Taarifa zimedai kwamba Meli hiyo ilianza kuzama saa 10 alfajiri baada ya kuingiza maji ndani na kukosekana kwa vifaa kama motor ya kutolea maji hayo kufikia saa 1 asubuhi hii Meli hiyo ilizama kabisa ndani ya maji.


Meli hiyo ilikuwa imebeba Dengu gunia 450 pamoja na Mbao zaidi ya 1000 huku wafanyakazi sita waliokuwa ndani ya Meli hiyo wakiokolewa.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ni meli ya mizigo mitupu na mabaharia mpaka sasa imeripotiwa kwamba wote ni wazima.


Source: Jamiiforums