Friday, 5 February 2010

Ofisi mpya ya Nahodha


Ofisi mpya ya Waziri kiongozi inayokamlishwa ujenzi wake huko Pemba. Kwa muda mrefu viongozi wengi wa SMZ wamekuwa hawapendi kwenda kufanya kazi zao katika kisiwa hiko. Kwa kukamilika kwa ujenzi huu kutatoa nafasi kubwa kwa Waziri Kiongozi kufanya kazi zake huko Pemba sawa na huko Unguja.

Aidha baada ya BLW kuridhia maridhiano ya Rais Amani na Maalim Seif, ni nafasi nzuri kwa Nahodha kuwepo muda mrefu kisiwani huko ili aweze kuzoeleka kwa wananchi wa huko, iwapo bado na ndoto za kuja kuwa Prez wa Zenj.

Awali Ofisi hiyo ambayo ilikuwa ikimfanya Nahodha kufikili mara mbili kabla ya kwenda huko ilikuwa kama inavyo onekana kwenye picha hii hapa chini...

Haikuweza kufahamika mara moja jengo hilo litatumika kwa shughuli gani mara baada ya Waziri Kiongozi kuhamia kwenye jengo jipya katika siku chache zijazo.

Thursday, 4 February 2010

Shujaa wetu:

Sunday, 31 January 2010

Nampuzika kuingia JF


Kwa muda wa miaka minne nimekuwa nikishiriki kikamilifu katika forum ya Jamii(JF). Kwa muda wote nilipokuwa katika forum hiyo nimeweza kujifunza mengi sana katika suala zima la ujenzi wa Taifa letu.

Binafsi nina blog yangu hii ambayo kwa muda mrefu nimekua nikiangalia kadhia mbalimbali hasa zinazohusu SMZ na Jamii nzima ya Tz visiwani. Hata hivyo sikuwa mbele sana katika kuona blog hii ikishiriki kikamilifu katika ujenzi wa Zanzibar, hii ni kutokana na kuweka nguvu zangu nyingi Jamii Forums.

Michango yangu ndani ya JF ilihusu sana suala zima la Visiwani na hatima yake, JF kama ukumbi huru umeweza kutoa nafasi kubwa kwa washiriki wake kujadili kwa kina kadhia mbalimbali zinazo zorotesha maendeleo ya Tanzania. Aidha kwa upande wa visiwani JF imekeuwa ikiota nasafi kubwa kwa kupokea michango mbalimbali juu ya hatima ya siasa za visiwani. Kwa hili napenda kuwapongeza sana watendaji wa JF na wachangiaji wa mada hizo.

Mimi binafsi nimewahi kuwa mtendaji katika SMZ, na nimeweza kukamilisha majukumu kadhaa yenye lengo ya kuboresha maisha ya watu wa visiwani. Majukumu hayo niliweza kuyafanya katika kipindi ambacho siasa za ubaguzi zilikuwa juu sana. Ubaguzi ambao ninaongelea hapa ni kuhusu Pemba na Unguja. Hapana shaka maelfu ya wapenda siasa wanajua kuhusu hili.

Hatua iliyofikiwa mwaka huu ya kuondoa tofauti za kisiasa ni jambo la kujivunia sana. Kitendo cha Mhe Karume na Maalim Seif kukutana kwa ajili ya kuondoa tofauti za kisiasa baada ya kushindwa kwa miafaka kadhaa sio jambo la kukebehi, ila ni mwanzo kwa kujenga upya Zanzibar iliyopotea kwa miaka zaidi ya therathini.

Pamoja nakejeli nyingi alizotupiwa Rais wa Zanzibar katika muda wake wa uongozi, ameweza kufanya yale ambayo hayakuwezwa kufanywa na mtu yoyote toka visiwani hadi bara. Rais Karume anamaliza muda wake, hata hivyo ataendelea kukumbukwa sana kwa hatua yake ya kuwa na maridhiano na CUF.

Sipendi kusema ni maridhinao, bali napenda kusema ni mapatano,kwani sasa ni wakati wa kuelewa na kufahamu siasa za Zenj hazitokai na chuki miongoni mwao bali chuki zilipandikizwa ili kuwezesha chama fulani kushika madalaka. Hivyo sio sahihi kusema ni maridhiano, kwani kwa kusema hivyo bado kutakuwepo na chuki binafsi miongoni mwetu.

Cha msingi ni kusema kuwa zanzibar sasa inaelekea kwenye mapatano ambayo jatajali Wakaazi wa visiwa hivyo zaidi ya itikadi zao za kisiasa. Na ni vema kwa wana visiwani wote kujua hilo na kushiriki kikamilifu katika kura za maoni ili kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Kwa muda mrefu nimekuwa mjumbe wa JF na nimeshiriki kikamilifu katika kutetea siasa za Zenj ikiwa ni pamoja na kuanzisha blog hii. Hta hivyo naona sasa ni muda muufaka wa kupumzika kuogelea siasa na kusubiri maamuzi muafakan ya wananchi wa Visiwani na hatima yetu kisiasa.

Nitaendele kupitia JF kwa kusoma janayojili pasipo kuchangia chochote.


Kwa muda huu napenda kuwajulisha wapenzi wote wa Vituko vya Zenj
kuwa tuwe pamoja katika ujenzi moya wa Zanzibar