Saturday, 6 February 2010

Maalim Seif kukutana na Watanzania UK,tarehe 13/02/10




Jumuiya ya Wazanzibar waishio Uingereza (ZAWA) ina furaha kuwaalika mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na Katibu Mkuu CUF Taifa, Maalim SEIF SHARIF HAMAD.

Wazanzibari na Watanzania wote waliopo UK na nchi za jirani wanakaribishwa kuhudhuria. Huu ni mkutano wa kwanza na wa kihistoria kufanyika hapa London baada ya maridhiano ya kuleta umoja miongoni mwa Wazanzibar.

SIKU: Jumamosi, tarehe 13/02/2010

WAKATI: Saa 7.30 mchana (1.30 PM)

PAHALA: Durning Hall (Nyuma ya Mangala Solicitor)
Earlham Grove,
Forest Gate, London
E7 9AB

Tel. 02085363800 (kupata maelezo ya mahala)

USAFIRI: Bus: 25, 86, 58 na Train: British rail (Forest Gate Station)

Friday, 5 February 2010

Ofisi mpya ya Nahodha


Ofisi mpya ya Waziri kiongozi inayokamlishwa ujenzi wake huko Pemba. Kwa muda mrefu viongozi wengi wa SMZ wamekuwa hawapendi kwenda kufanya kazi zao katika kisiwa hiko. Kwa kukamilika kwa ujenzi huu kutatoa nafasi kubwa kwa Waziri Kiongozi kufanya kazi zake huko Pemba sawa na huko Unguja.

Aidha baada ya BLW kuridhia maridhiano ya Rais Amani na Maalim Seif, ni nafasi nzuri kwa Nahodha kuwepo muda mrefu kisiwani huko ili aweze kuzoeleka kwa wananchi wa huko, iwapo bado na ndoto za kuja kuwa Prez wa Zenj.

Awali Ofisi hiyo ambayo ilikuwa ikimfanya Nahodha kufikili mara mbili kabla ya kwenda huko ilikuwa kama inavyo onekana kwenye picha hii hapa chini...

Haikuweza kufahamika mara moja jengo hilo litatumika kwa shughuli gani mara baada ya Waziri Kiongozi kuhamia kwenye jengo jipya katika siku chache zijazo.

Thursday, 4 February 2010

Shujaa wetu: