Wakimbizi wa Kizenj, karibuni tena Zanzibar
Wale wanzenji wote waliokimbimba Zanzibar kutokana na mtafuruku wa uchaguzi wa mwaka 1995 na mwaka 2000, mnakaribishwa tena Zanzibar.
Zanzibar ya leo ni tofauti sana na ile mliyoikimbia. Sasa kuna makubaliano na kutakuwepo na serikali ya umoja wa kitaifa mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu. Hivyo basi sio sahihi tena kujiita wakimbizi ilhali hali ya nchi ni shwari.
Aidha naiomba serikali ya Uingereza kuwarudisha wazenj wote waliongia nchini humo kwa madai ya ukimbizi, ombi hili ni pamoja na serikali ya Kenya ambako kuna wakimbizi wa kizenj katika mapango huko Mombasa.
Sina shaka kuwa Wazenj wa UK wengi wao wamepata bahati ya kusoma huko na kuwa na taaluma, hili ni muhimu kwa kujenga taifa jipya la Zanzibar... Kule mapangoni sina hakika kama waliweza kupata nafasi ya kujiendeleza.
Cha msingi kwenu wakimbizi wa kisiasa ni kurudi nyumbani, kwani hakuna vujo tena, kura zenu tunazihitaji hali kadhalika maarifa yenu. Hii ajialishi kama ukuweza kufanikiwa huko ugenini.
Karibuni tena nyumbani, tena mjisikie huru kuliko huo uhuru wa kubaguliwa katika nchi za kigeni. Karibuni sana