Monday, 20 November 2006

SMZ na Vilabu vya Pombe...

Pengine ni Zanzibar pekee katika Afrika Mashariki ambako unaweza kukuta Mahakama ya Vileo. Mahakama hii hufanya kazi chini ya Waziri wa Tawala za Mikoa, ikiwahusisha Wafanyakazi toka katika Mahakama ya wilaya, Baraza la Manispaa na Waombaji wa leseni ya kuuza vileo katika kisiwa cha Zanzibar.

Mahakama hii ipo siku nyingi zaidi ya uhai wa SMZ yenyewe, aidha imekuwa ikizidi kupata umaarufu siku za karibuni, ambako kumekuwepo na pingamizi za wazi kuhusu uhanzishwaji wa vilabu vya pombe na suala zima la unywaji pombe visiwani humo.

Pingamizi kubwa toka kwa wananchi ni kwamba vibalu vingi vimekuwa vikianzishwa karibu na nyumba za ibada na sehemu za maakazi ya watu. Hivyo kuwepo na kero kwa wananchi kutokana na kelele za wanywaji au pilikapilika za kwenye vilabu hivyo.

Hata hivyo sio wananchi wengi ambao wanajua shughuli za Mahakama hii, hivyo wengi wao huishia kutupa lawama zao kwa Baraza la Manispaa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Kwa ufupi Mahakama hii hukutana mara moja kwa mwaka kupitisha maombi yote ya uanzishaji wa biashara ya ulevi, kuongeza muda kwa lesini za biashara ya ulevi, kufuta lesini zilizoshindwa kufuata utaratibu n.k Mahakama hii haiusiki na utoaji wa vibali vya ujenzi wa nyumba za ulevi.

Hivi karibuni Mh. Waziri wa Tawala za Mikoa Visiwani humo aliitaka mahakama hiyo kutotoa leseni kwa vilabu vya ulevi vilivyopo karibu na Maakazi ya watu na nyumba za ibada, na ni baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi toka kwa wananchi.

Pengine ni wakati ambao tunapaswa kujiuliza kuwa ni sehemu zipi za maakazi ya watu, ni sehemu zipi za biashara ni sehemu zipi za elimu ni sehemu zipi za viwanda na ni sehemu zipi za kilimo ndani ya kisiwa hicho. Kwa haraka haraka sio rahisi kujua hilo na hasa ikizingatiwa hali halisi ya mpango wa mji wa kisiwa hicho. Hata ukiangalia master plan ya Mwaka 1982 chini ya Sheria ya Ardhi ya mwaka 1985, haikuweza kuweka bayana sehemu maalumu kwa ujenzi na uendeshaji wa biashara ya ulevi. Masterplan hiyo ilitenga maaeneo ya Maakazi, Viwanda na Elimu tu. Hivyo basi leo hii kusema kudai kuwa Vilabu visiwe katika maaneo ya wakaazi sio sahihi.

Zaidi wenye vilabu na wanywaji wa ulevi katika kisiwa hicho, ni wastaraabu sana na ni watu ambao wanajua kuheshimu uhumimu wa kuheshimu Majirani zao, iwe ni sehemu ya Ibada au Maakazi ya watu.
Kwa mfano, kila inapokaribia adhana, basi redio au muziki ndani ya kilabu huzimwa hadi adhana inapokwisha. Kwa maelewano mazuri kati ya wenye baa na baadhi ya misikiti iliyokaribu na baa hizo huweza kusaidiana huduma ya maji, na hasa kwa waumini kwenda kutawadha katika baa pasipo usumbufu wowote. Hivyo ni vema kuendelea kuheshimu uungwana wa walevi wa visiwa hivyo ambao ulevi wao ni wa kistaarabu kuliko walevi wa nchi nyiongi dinuani

5 comments:

SIMON KITURURU said...

Duh!Asante kwa habari hii!

Mija Shija Sayi said...

Kesi hii ngumu! Lakini kwa vile walishakosea toka mwanzo kutoa viwanja bila mpangilio itabidi wavumiliane.

mwandani said...

Haya - kuchota maji ya kutawadha kwenye baa - sijui tuanze na wapi.

wazee wa tawala za mikoa bora wafikirie kuanzisha biashara ya vifaa vya sound-proofing halafu waweke mkakati kila baa ikarabatiwe na vifaa hivyo kabla ya kuongeza muda wa leseni.
kwa sasa waendelee kustahimiliana.

ndesanjo said...

Sikujua kuwa Tanzania tuna mahakama za vileo. Sishangai pia wananchi wengi hapo visiwani hawaifahamu. Habari mpya kwangu hii.

Che Guevara Mwakanjuki said...

Mahakama ya vileo ipo, zamani zanzibar mtu kuingia baa na kuweza kunywa pombe alihitaji kuwa na leseni..
Baadae sheria hiyo iliondolewa, lakini Mahakama hiyo iliendelea kuwepo kwa kutoa leseni kwa mtu yoyote ambae anahitaji kufanya biashara ya ulevi kisiwani humo.