Wednesday, 11 April 2007

Safarini Uingereza

Wapenzi wa kona hii ya Vituko vya Zenj, napenda kuwataarifu kuwa nitakuwa safarini Uingereza kuanzia mwishoni mwa wiki hii..

Kwa miezi kadhaa ijayo nitakuwa na blog tokea jiji la London. Zaidi itakuwa jambo la msingi iwapo nitaweza kukutana na wanablog wa Uingereza...na watanzania wengine ambao ni wapenzi wa blog..

3 comments:

SIMON KITURURU said...

Safari njema mzee!

kibunango said...

shukrani... summer ya finland nakuachia mwenyewe..

kibunango said...

Nimefika salama kabisa Hapa UK.. Na nimependa mapokezi ya vijana wa hapa UK... Ni mazuri na yakuvutia... Jana ilikuwa siku ya joto kali kabisa hapa UK, shukrani nilikuwa beach nikituliza koo kwa bia baridi sana.

Jioni nilikwenda kumpokea dada mmoja toka Tanzania.. Bahati mbaya alishindwa kujieleza kwa uhamiaji hivyo kushindwa kuingia UK... Baada ya masaa matano ya kumsubiri tulipata taarifa kuwa anarudishwa tz na ndege ya asubuhi..