Sunday 8 March 2009

Nani Mjinga Hapa?


Pichani ni mwanamke wa kizenj akiwa katika pilika pilika zake ufukweni, na pembeni kushoto ni mtalii akicheza na maji.

Jaribu kuangalia tofauti ya mavazi kati ya wanawake hawa wawili, halafu jaribu kufikilia hali ya hewa ya Zanzibar, bila kusahau udhaifu wa ngozi za watalii dhidi ya jua kali la ikweta.

Je unafikili kati ya hawa wanawake ni nani mjinga kutokana na aina ya mavazi yake?

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

hapo inategemea kwasababu sizani kama huyo mzenj angependa kuvaa kama mtalii na pia sidhani mtalii angependa kuvaa kama mzenj. Kwa hiyo mi sioni kama kuna mjinga.

Aliko said...

Hapa kuna clash of cultures! miaka ya nyuma ufukwe yaani Beach uliuzwa kwabei ya kutupa ikifirika kama utalima nini mchangani.. mzungu analipa dola nyingi kwenda kulala nusu uchi hapo juani, Dada wa kizenji anatafuta hijabu na kanga nyingi kujikiga na jua.... sanaa ya picha hii inaonyesha utofauti mkubwa uliopo kati ya wazung wa kike na Dada zetu

Kaziyabure said...

hakuna mjinga,kila mtu na ustaarabu wake,wakizungu vichupi,wakizenji 'kujisitiri'.

Anonymous said...

Swali halina msingi, linasahau kwamba wote wawili wanatoka katika tamaduni tofauti na kama unajaribu kuzungumzia kujikinga basi wote inawezekana wanajikinga kwa jua kwani kuwa karibu na ikweta si lazima utakapokuwa kukujifunika ni lazima uathirike na mionzi kwani unaweza ukatumia mafuta ya kujikinga na jua. Hivi karibuni nimetembelea hospitali ya Ocean Road na kukuta kesi nyingi sana za kansa ya ngozi ambapo wengi wetu tumekuwa tukifikiri kuwa kuvaa shati la mikono mirefu ama baibui linakinga mwili, hii si kweli. Hivyo nakubaliana na wote wanaosema hakuna mjinga bali swali lako linashindwa kueleweka.