Friday 6 March 2009

Maji ya Karume Bai bai, Karibu maji ya Japan



Kwa muda mrefu kisiwa cha Zanzibar kimekuwa kikipata huduma ya maji bure, hatua ambayo ilitokana na mapinduzi ya mwaka 1964. Huduma hiyo muhimu kabisa katika maisha ya kila siku ya binadamu ilibatizwa jina na kuitwa maji ya Karume. Hata hivyo jina hilo halikuja burebure tu! kuna sababu kadhaa ambazo zilisababisha maji hayo yaitwe ya Karume. Moja ya sababu kubwa ilikuwa ni upungufu wa maji na hasa katika halmashauri ya manispaa ya Zanzibar,ambapo wananchi wengi walijikuta wakitafuta maji sehemu mbalimbali za manispaa hiyo. Usumbufu wa upatikanaji wa maji ulisababisha maji hayo kuitwa Maji ya Karume ambayo yalikuwa ni bure lakini shida kupatikana.

Maendeleo yote yaliyotokana na mapinduzi yaligeuka kuwa adha na kero baada ya maji kupungua katika manispaa, Majengo kama ya Mjeru pale Kikwajuni ambayo yalikuwa yakipata maji muda wote yalijikuta yakikosa maji muda mwingi wa mchana na maji yaliweza kutoka usiku tu, na ni usiku wa manane, hivyo kuwafanya wakaazi wake kubadilisha ratiba ya kulala ili waweze kukinga maji. Hali hii ilikuwepo kwa maeneo ya Kilimani, Michenzani na sehemu kadha wa kadha katika manispaa hiyo.

Ukosefu wa maji ya kutosha katika maeneo hayo ambayo yalikuwa na nyumba za ghorofa kulisababisha kubadilika kwa sura za majumba hayo kwa uwekaji wa pump za maji,nyingi katiya hizo kufungwa kienyeji tu na kuendelea kuwa kero kwa wananchi hao. Aidha uchimbaji wa makaro makubwa ya kuhifadhia maji chini ardhi ulishamiri na kupunguza upatikanaji wa maji hayo machache/kidogo kwa wakaazi wengine. Uchimbaji wa visima vile vile ulishamiri kando kando ya manispaa hiyo. Hii yote ilitokana na upungufu mkubwa wa maji ya Karume.

SMZ kwa upande wake walijitahidi kuona kero hiyo inaondoka, lakini mara zote miradi ya maji yenye nia ya kuwa endelevu ilishindwa kuendelea kutokana na SMZ kuendelea kupendelea kuwa na Maji ya Karume.

Wananchi kwa upande wao walikuwa tayali kulipia huduma za maji,hii inaonyeshwa na mifao kadhaa ya baadhi ya wananchi walioamua kutafuta njia za kudumu za upatikanaji wa maji katika maeneo yao. Miradi mingi midogo midogo ya maji iliyowashirikisha wananchi ilifunguliwa na mingi katika hiyo ilitumika kama mifano katika hatua za awali za semina mbalimbali za kubadili msimamo wa serikali na maji yao ya Karume.

Maji ya Karume yalianza kuaagwa rasmi tokea mwaka jana, hata hivyo sio wananchi wote ambao wameweza kupata maji ya Japan licha ya Idara ya maji kuwatumia ankara za maji. Hii kwa upande mmoja inaonyesha kuwa Idara ya Maji bado haijawa makini katika kuona kuwa maji yanalipiwa na yule tu ambae mfereji wake haukauki maji, na sio wale wenye mifereji iliyokauka au ile yenye kupiga filimbi kama maji yanakuja kumbe la..!

Udhaifu huu unathibitishwa na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi,Bw, Mansour Yussuf Himid katika kauli yake aliyoitoa hivi majuzi wakati wa kusaini awamu ya pili ya maji ya Japan

``Napenda kutoa wito kwa wale wanaopata huduma ya maji kukubali kuchangia na wale wasiopata hawatatozwa fedha hadi hapo watakapoanza kupata maji ya uhakika,``

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Maji ni muhimu kwa kila binadamu. kakangu nakumiss kwani ni siku nyingi sijakuona ku nitembelea vp

Kibunango said...

Nimekuwa napita mtaani kwako kama kawaida, ila kwa ukimya kidogo. Anyway nitaanza kupita kama zamani kwa kelele nyingi na vishindo tele...:)

Aliko said...

Anonymous hapo juu kamwaga manyanga chini si utani.. if any of that is true basi ze utamuz kafichuliwa...
Maji ni Uhai chakushangaza Zanzibar ilikua kisiwa uhai wakati wa mashua karne zilizo pita kwani maji yalipatikana hapo kwa mabaharia wa safari ndefu... umuhimu wakuyalipia kwa karne haukwepeki ttokana na kupanda kwa gharama za maisha ulimwenguni kote.

Anonymous said...

First of all.u and all of u.u should know there and there was no "maji ya karume".speak the truth.
water was free in that Island since my great grandpa was born,my daddy and me and my sons.
So dont bring your maji ya karume here.so the education and the treatment toooooooo.

Man.ask the neighbours for ze ghord.
u catch me?????????.

Paul said...

Hello, I'm having trouble finding what "wakati wa mashua" means. I was told it means "dry season" or "season of dry" but in a dictionary it said "mashua" means 'launch' or 'a medium sized boat.' Could you tell me the meaning of this phrase and how it is used in speech? thanks!

(I know this isn't what you are talking about but this page came up on a google search)

Kibunango said...

Paul;
Sina hakika unataka kuitumia vipi hiyo "wakati wa mashua" katika speech yako. Aidha kulingana na mada hii, wakati wa mashua unarudi nyuma hadi karne ya 18 ambapo kulikuwa na mashua nyingi zitumika katika biashara baina ya bara na visiwani.

Watumiaji wa mashua hizo waliweza kunufaika moja kwa moja na maji safi na bora ya Zenj, na wengi walitumia kisiwa hicho kama kituo cha kuongeza akiba yao ya maji katika mashua zao