Tuesday, 18 August 2009

Hamad Masauni, na Siasa za kukariri...Anavyosema kuhusu Pemba ni tofauti sana na hali halisi ya huko Pemba..

Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, Hamad Masauni Yusuf alisema ingawa hajui vigezo vilivyotumika katika utafiti, anaamini kuwa wananchi wengi bado wana kasumba kwamba CUF bado ina ngome kubwa kisiwani Pemba wakati hali sasa ni kinyume.

Alisema sio kweli kwamba, CUF wana nafasi kubwa ya kushinda urais kwa Zanzibar na pia huko Pemba na kwamba hali imebadilika kwa sasa akidai kuwa, wananchi wengi wamekata tamaa na viongozi wao na hivyo, CCM ina nafasi kubwa ya kushinda.


Kauli hizi na hali halisi ya huko Pemba ni sawa na kujisuta

2 comments:

Kaziyabure said...

Hawaijui Pemba hao,watuulize siye tuliyekuwa na Makaazi huko.
Ngome ya CUF Pemba ni kubwa sana,hata wale wanaojifanya ni maCCM katika mioyo yao ni MACUF,ngome ile..labda,labda inaweza ikayumba siku na kipindi Maalim Seif atakapoondoka Duniani tena nasema Labda!

kibunango said...

Nafikiri Hamad anatakiwa aende huko Pemba katika kipindi hiki, na akae huko sio chini ya miezi mitatu akisoma na kushiriki katika shughuli zote za kijamii na kichama kabla ya comments zozote juu ya uimara wa CCM huko PBA....

Siasa za kukurupuka na kukariri zimepitwa na wakati!