Sunday 31 January 2010

Nampuzika kuingia JF


Kwa muda wa miaka minne nimekuwa nikishiriki kikamilifu katika forum ya Jamii(JF). Kwa muda wote nilipokuwa katika forum hiyo nimeweza kujifunza mengi sana katika suala zima la ujenzi wa Taifa letu.

Binafsi nina blog yangu hii ambayo kwa muda mrefu nimekua nikiangalia kadhia mbalimbali hasa zinazohusu SMZ na Jamii nzima ya Tz visiwani. Hata hivyo sikuwa mbele sana katika kuona blog hii ikishiriki kikamilifu katika ujenzi wa Zanzibar, hii ni kutokana na kuweka nguvu zangu nyingi Jamii Forums.

Michango yangu ndani ya JF ilihusu sana suala zima la Visiwani na hatima yake, JF kama ukumbi huru umeweza kutoa nafasi kubwa kwa washiriki wake kujadili kwa kina kadhia mbalimbali zinazo zorotesha maendeleo ya Tanzania. Aidha kwa upande wa visiwani JF imekeuwa ikiota nasafi kubwa kwa kupokea michango mbalimbali juu ya hatima ya siasa za visiwani. Kwa hili napenda kuwapongeza sana watendaji wa JF na wachangiaji wa mada hizo.

Mimi binafsi nimewahi kuwa mtendaji katika SMZ, na nimeweza kukamilisha majukumu kadhaa yenye lengo ya kuboresha maisha ya watu wa visiwani. Majukumu hayo niliweza kuyafanya katika kipindi ambacho siasa za ubaguzi zilikuwa juu sana. Ubaguzi ambao ninaongelea hapa ni kuhusu Pemba na Unguja. Hapana shaka maelfu ya wapenda siasa wanajua kuhusu hili.

Hatua iliyofikiwa mwaka huu ya kuondoa tofauti za kisiasa ni jambo la kujivunia sana. Kitendo cha Mhe Karume na Maalim Seif kukutana kwa ajili ya kuondoa tofauti za kisiasa baada ya kushindwa kwa miafaka kadhaa sio jambo la kukebehi, ila ni mwanzo kwa kujenga upya Zanzibar iliyopotea kwa miaka zaidi ya therathini.

Pamoja nakejeli nyingi alizotupiwa Rais wa Zanzibar katika muda wake wa uongozi, ameweza kufanya yale ambayo hayakuwezwa kufanywa na mtu yoyote toka visiwani hadi bara. Rais Karume anamaliza muda wake, hata hivyo ataendelea kukumbukwa sana kwa hatua yake ya kuwa na maridhiano na CUF.

Sipendi kusema ni maridhinao, bali napenda kusema ni mapatano,kwani sasa ni wakati wa kuelewa na kufahamu siasa za Zenj hazitokai na chuki miongoni mwao bali chuki zilipandikizwa ili kuwezesha chama fulani kushika madalaka. Hivyo sio sahihi kusema ni maridhiano, kwani kwa kusema hivyo bado kutakuwepo na chuki binafsi miongoni mwetu.

Cha msingi ni kusema kuwa zanzibar sasa inaelekea kwenye mapatano ambayo jatajali Wakaazi wa visiwa hivyo zaidi ya itikadi zao za kisiasa. Na ni vema kwa wana visiwani wote kujua hilo na kushiriki kikamilifu katika kura za maoni ili kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Kwa muda mrefu nimekuwa mjumbe wa JF na nimeshiriki kikamilifu katika kutetea siasa za Zenj ikiwa ni pamoja na kuanzisha blog hii. Hta hivyo naona sasa ni muda muufaka wa kupumzika kuogelea siasa na kusubiri maamuzi muafakan ya wananchi wa Visiwani na hatima yetu kisiasa.

Nitaendele kupitia JF kwa kusoma janayojili pasipo kuchangia chochote.


Kwa muda huu napenda kuwajulisha wapenzi wote wa Vituko vya Zenj
kuwa tuwe pamoja katika ujenzi moya wa Zanzibar

Thursday 28 January 2010

BLW: Hoja ya Serikali ya Kitaifa Yawasilishwa Leo...




Dondoo 5 za hoja ya msingi ni -

1. BLW liyaridhie na kuyapa nguvu Maridhiaano.

2. Uanzishwe mfumo serikali ya Umoja wa Kitaifa itayohusisha vyama vya siasa vyenye wajumbe ndani ya BLW.

3. Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa izingatie uwiano kwa mujibu wa kura za urais.

4. Baraza lifanye marekebisho ya vifungu vya 39, 42 na 62 ili kuweka utaratibu wa serikali ya Umoja wa kitaifa.

5. Baraza liweke utaratibu wa kura za maoni, referendum.


Source: JF

Tuesday 26 January 2010

Maridhiano: Alichosahau Maalim Seif...


Maalim Seif katika taarifa yake ya Maridhiano na Mustakbali wa Zanzibar, amezungumzia mengi juu ya Zanzibar ilipotoka hadi ilipo sasa. Cha ajabu hakuzungumzia kabisa juu ya kuwepo kwa utumwa visiwani humo, kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.

Sunday 24 January 2010

Maridhiano: Sasa yaandaliwa sherehe...



CUF kusherehekea ushindi

Wakati hali ya kisiasa Visiwani ikiingia katika historia mpya, taarifa zilizopatikana mjini hapa zimedai kuwa Chama cha CUF kinafanya maandalizi ya kusherehekea ushindi baada ya kufanikiwa kuwashawishi baadhi ya vigogo wa CCM Zanzibar kukubali kuundwa kwa Serikali ya mseto kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.

Katika maandalizi hayo ambayo inasemekana yanafanyika kwa usiri mkubwa, viongozi wa CUF wanaelezwa kukubaliana na mapendekezo ya Baraza la Mawaziri ambalo litajumuisha na wenzao wa CCM katika Serikali ya muda itakayoongozwa na Rais wa sasa wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

Chanzo cha habari hizi kimedai kuwa chini ya mapendekezo hayo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad atakuwa Waziri Kiongozi nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Shamsi Vuai Nahodha ambaye anakusudiwa kutupwa nje ya Baraza jipya la Mawaziri.

Wengine waliopendekezwa na Wizara zao zikiwa kwenye mabano ni Mansoor Yussuf Himid–CCM (Mafuta na Nishati), Samia Suluhu Hassan-CCM (Afya), Juma Dui Haji – CUF (Biashara Utalii na Uwekezaji), Nassor Mazrui-CUF (Fedha), Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini-CCM( Kilimo, Ardhi na Maji).

Wengine ni Fatma Abdulhabib Ferej-CUF (Wanawake, Watoto Maendeleo ya Vijana), Burhan Saadat Haji-CCM (Mawasiliano), Machano Othman Said-CCM (Waziri wa Tawala za Mikoa na Vikosi Maalum), Asha Abdulla Juma-CCM (Elimu), Abbas Juma Muhunzi-CUF( Ofisi ya Waziri Kiongozi), Ali Juma Shamuhuna – CCM (Ofisi ya Rais).

Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakar amependekezwa kuwa Waziri wa Katiba na Utawala Bora.

Chanzo hicho kimedai kuwa mapendekezo hayo ya Baraza la Serikali ya muda yamekuwa yakisambazwa kwa vigogo wa CUF tu ikiwa ni ishara kwao ya ushindi wa suala walilokuwa wakilitaka la kuwepo ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Pamoja na hali hiyo, kundi la wajumbe ambao wanapinga harakati hizo ni kubwa na ambalo linaundwa na wanasiasa wenye ushawishi mkubwa wa siasa za Tanzania na kwa namna hali inavyokwenda kikao hicho cha Kamati Maalum kitatawaliwa na vijembe vingi na upinzani mkali kwa watu waliopachikwa jina la ‘Uhafidhina’.

Tayari Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi Abubakar Khamis Bakar ameshawasilisha hoja binafsi kwa Katibu wa Baraza akitaka kufanyike marekebisho ya katiba yatakayoruhusu kubadilisha mfumo wa utawala wa SMZ kwa kuwa na Serikali ya mseto.

Idadi kubwa ya wafuasi wa CCM na viongozi wamekuwa wakipinga suala la kuongezwa muda kwa Rais Karume pamoja na kuwepo kwa Serikali ya mseto Zanzibar wakidai kuwa mazingira hayaruhusu kwa uundwaji wa serikali hiyo na kusisitiza msimamo wa utekelezaji wa azimio la CCM Butiama.