Tuesday, 23 January 2007

Nungwi : Ukahaba, Nguo fupi na Ulevi hauna nafasi..

Linapokuja suala la ukahaba, Kijiji cha Nungwi huko Zanzibar kimekuwa mbele kukanya tabia hizo wazi wazi. Wamejaribu kutumia njia mbalimbali ikimemo maandamano, risala na kutimia viongozi wao katika kukemea tabia hiyo, hali hiyo ni tofauti kidogo na mjini Zanzibar ambapo makundi ya vijana hujichukulia sheria mkononi kuwahadhibu makahaba na wale wavao nguo fupi.
Hatua iliyochukuliwa mwanzoni mwa wiki hii na Kamati ya Maadili na Maendeleo katika kijiji cha Nungwi ya kutunga sheria ndogo ya kudhibithi uvaaji nguo fupi, ukahaba na ulevi inathibitisha ni kwa jinsi gani wanakijiji hicho hupenda kupita katika njia zinazokubalika katika kutoa kero zao.
Nikirudi nyuma na kuangalia kile kinachodaiwa kuwa ni ukahaba na mambo mengine yanayokwenda tofauti na maadili ya wakaazi wa Nungwi, yalianza mara baada ya kijiji hicho kukaribisha hoteli za kitalii. Kabla ya kuja kwa hoteli za kitalii kijiji hicho kilikuwa ni maarufu kwa uundaji wa majahazi na shughuli za uvuvi.
Miaka ya tisini ambayo ilikuwa ni ya mabadiliko makubwa katika sekta ya utalii visiwani huko, Waakazi wa Nungwi walishuhudia maandamo ya kinamama kupinga kuwepo kwa wanawake na wasichana toka mkoani Tanga ambao walidaiwa kuwepo huko kwa lengo la kufanya ukahaba. Wakinamama hao walidai wadada hao toka Tanga wamekuwa wakiwarubuni waume zao na kufanya nao mapenzi kwa pesa na kusababisha hali ngumu katika nyumba zao. Waliendelea kwa kusema uwepo wao hapo kutasababisha kuongezeka kwa ukimwi na kupolomoka kwa maadili. Hivyo waliwataka akinadada hao kuondoka mara moja kijijini mwao. Hatua yao hiyo ambayo iliungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, ilizusha mjadala mrefu kuhusu nafasi ya Wabara katika visiwa hivyo. Zaidi ilionekana kuwa Watz bara wanazuiwa kutumia haki yao ya msingi ya kwenda popote pale ndani ya Tanzania pasipo bughuza. Hata hivyo maandamano hayo yalishuhudia kuongezeka kwa Watanga ambao sasa walihamia mjini na vijiji vingine vyenye hoteli za kitalii.
Nungwi hawakuishia hapo, wakanyosha vidole kwa wageni wengine ambao ni wafanyakazi wa mahoteli kwamba wanavaa nguo fupi na suruali za kubana. Kipindi hicho wafanyakazi wengi katika hoteli za kitalii huko walikuwa ni wananchi toka Kenya.
Hatua za Kamati hiyo ya kutunga sheria ndogo ndogo za kudhibiti uvaaji wa nguo fupi na ukahaba, ni hatua nzuri katika kulinda maadili yao. Hata hivyo kuna vitu kadhaa vya kujiuliza juu ya uhalali wa sheria hizo ndogo ndogo na hasa katika kuzisimamia na utekelezaji wake. Kimsingi kuhusu uvaaji wa nguo fupi, kamati hiyo inawataka wale wote wavaao nguo fupi kuvaa vazi la Kizanzibari. Vazi la kizanzibari kwa ufahamu wangu ni kuvaa kanga zaidi ya mbili, huku ukiwa umefunika sehemu zote za mwili na kuachia sura tu. Sheria hii inaweza isikubalike kwa wengi wa wafanyakazi katika hoteli hizo ambao sio wenyeji wa zanzibar.
Na iwapo vazi la kizanzibari ni kama lile la kuvaa baibui na hijabu yake, basi sheria hiyo itakuwa inalenga zaidi maadili ya kidini kuliko maadili ya kizanzibari, na itakuwa sio kosa kuhoji kauli ya serikali ya kusema kuwa nchi hiyo si ya kidini. Na kwanini wananchi ambao sio wa dini fulani washurutishwe kuvaa baibui?
Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kaskazini ambayo ndio imepelekewa sheria hizo ili izibaliki, kabla ya Sheha na Wajumbe wake kuanza kucharaza viboko hadharani kwa dada zetu, itabidi iipitie vizuri sheria hizo kabla ya kuziruhusu kutumika. Lengo ni kuona haki sawa kwa waakazi wa kijiji hicho na kisiwa cha zanzibar kwa ujumla, inazingatiwa.

10 comments:

Kaziyabure said...

Brother K, mimi hawa watu wa Nungwi huwa siku zote wananishangaza,wanapenda kufanya vitu vyao kibinafsi utafikiri ardhi au eneo hilo waliandikiwa kutoka mbinguni kuwa ni lao. Waelewe Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hivyo wasitake kuwanyanyasa hao wananchi kutoka bara.
Viongozi wa nungwi mara wengi wao ni mbumbumbu na cha ajabu maamuzi yao ya kimbumbu huwa yanapata mwega kutoka kwa viongozi wa juu serikalini kama Juma Shamhuna. Kama ni kiongozi mwenye elimu lazima angeelewa vijisheria vyao vyote wanavyovipitisha viko kinyume na katiba ya Zanzibar na ile ya URT.. kwa mfano katiba ya zanzibar katika Ibara ya 5 inasema na nanukuu...."Zanzibar shall be a state of multiparty democracy which shall uphold the rule of law, human rights, equality, peace, justice and equity". Sasa kama katiba inalazimisha kutekeleza haki za kibinaadamu kwa nini wao wanataka kuvunja haki hizo kumchagulia mtu vazi la kuvaa n.k?? Hivi hawajui kwamba zanzibar pia inabanwa na sheria za kimataifa za haki za kibinadamu?

Simon Kitururu said...

Naelewa kwanini Wanakijiji wanataka sheria ipitishwe.lakini ikipita nafikiri kuna baadhi ya watalii weusi watakao ipata kwa kukosea kuvaa.Hii sheria itawahusu hata wamagharibi wanaopenda kujianika kwenye jua kupata ukahawia?Rafiki yangu mmoja ameniambia alipotembelea mitaa ya Tunisia na hata Misri alikuta kuna baadhi ya sehemu walikuwa wana matatizo kama haya.Wakajaribu kutenga maeneo ambayo watalii huruhusiwa kutembea na bikini na kunywa pombe.Lakini huruhusiwi kuvuka mpaka

Anonymous said...

Imani za kidini zikianza kutungiwa sheria na serikali zisizo za kidini, lazima watu tuanze kuuliza maswali. Maadili yakianza kufunzwa kwa kutumia bakora kama Afganistani au Somalia, tunakuwa kama vile tunaishi miaka 200 iliyopita. Kuna njia nyingi bora zaidi za kufunza maadili, tena toka utotoni, kupitia mfumo wa elimu, vyombo vya habari, dini, n.k. Kujenga mwanadamu mwenye maadili yanayotoka ndani na sio maadili kebehi na ya kinafiki kwa kuogopa bakora.

Ajabu ni kuwa mara nyingi mambo ya maadili huwa yanaathiri zaidi wanawake. Tunaona kule Nigeria baada ya kupitishwa sheria ya kuuawa kwa zinaa, wanaopatikana na hatia ni wanawake (wanapopata mimba).

Mimi nilidhani kuwa dini hizi za kuja zinatuambia kuwa kuna siku ya adhabu. Kuna mahali panaitwa jehanamu ambapo wenye dhambi wataunguzwa moto wa milele na mungu mwenye huruma na upendo usio na kifani!

Anonymous said...

Kaka Chege, nashukuru kwa kunijibu, Ila nimesikitika sana kusikia kuhusu Fanon! Pole sana,na tafadhali nifikishie pole nyingi sana kwa familia nzima huko nyumbani.Nashindwa kuamini kabisa. Lakini ndio kazi ya Mungu, yeye hutoa na yeye hutwaa. Samahani kwa kuandika yote haya kwenye blog, sioni email yako.
Mimi email yangu ni subiraga@sbcglobal.net.
Asante,

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Kibunango said...
This comment has been removed by the author.
MTANZANIA. said...

Samahani ndugu, Natoka nje ya mada kidogo. Nasikia Fanon ametutoka. Tuwekee details kidogo kama unajua lolote juu ya kifo chake. Vile vile karibu kwenye blog yangu. Asante.

Simon Kitururu said...

Che!Hivi RS ndio nini?Egdio kanistua kuwa wewe unaijua.

Kibunango said...

Mtanzania, Hiyo habari ni ya kweli, aidha nitakuandikia katika e-mail.

Simon..
Naona giza hapo!!!

matusi said...

nashangaa mbona hamsemu kuhusu hao walotoka unguja na wanacheza sinema za matusi UK?

HUAMINI BASI BONYEZA HAPA

http://videozamatusi.blogspot.com/