Friday, 8 June 2007

'Ongezeko la Uzaaji UK' Wazenj Hawako Nyuma....

Imeripotiwa kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la uzaaji hapa UK, ikiwa ni ongezeko kubwa kwa miaka 26. Ongezeko hilo la uzaaji, limechangiwa na wahamiaji miongoni mwao wakiwa ni wazenj.

Moja kati ya watoto watano wanaozaliwa hapa, amezaliwa na mhamiaji, hivyo kufanya ongezeko la asilimia kumi kwa mwaka kwa watoto wanaozaliwa na wahamiaji. Mwaka 2006 walizaliwa watoto 669,531 kwa wastani wa kila mzazi wa 1.87 huku wahamiaji wakizaa asilimia 21.9 ya watoto wote waliozaliwa mwaka 2006. Wahamiaji wengi ni kutoka nchi za ulaya ya mashariki, wengi wao wakiwa ni Wapoland. Zaidi kumekuwepo na ongezeko kubwa watoto toka kwa wanawake wa Pakistan, India, Afrika na Mashariki ya Kati. Wachunguzi wa mambo wanasema tokea mwaka 1997 (labour ilipoingia madarakani) kiasi cha wahamiaji milioni 1.5 wamehamia UK.[1]

Wanawake wengi toka Zenj hawapo nyuma katika suala la uzaaji, wengi wa wanawake hao ni kinamama wa nyumbani. Nilipojaribu kuulizia zaidi kuhusu uzaaji huo wa kasi, wengi wao walisema ni kutokana na mafao mazuri ambayo hutolewa na serikali ya hapa, hivyo kutokuwa na wasiwasi juu ya malezi na usomeshaji wa watoto hao tofauti na kama ingekuwa huko Zanzibar, ambapo jukumu lote lipo kwa mzazi pekee..!



1.Source: Daily Mail, June 8 2007.

2 comments:

Anonymous said...

hebu tuwekee takwimu katika hii population growth ya UK, hao Wazenj ni asilimia ngapi? na Jee kweli wamezaa zaidi dhidi ya wanawake wengine wa east africa hapa UK? waganda, wakenya,rwanda, warundi nk? acha agenda zako dhidi ya wazanzibari njoo na fact sio ubabaishaji.

Kibunango said...

Jaribu kutafuta gazeti la Daily Mail ambalo nimenukuu. Aidha Takwimu halisi ya Wazenj inajumuisha Waburundi, Wasomali, wanyarwanda n.k Kwani wengi wa Wazenj sasa sio wananchi wa Zanzibar...