Saturday, 18 April 2009

Kisauni Airport kuongezwa kwa mita 560


Zanzibar International Airport maarufu duniani kama Kisauni Airport inatazamiwa kuongezwa urefu wa njia yake kwa mita 560. Ni katika mradi uliopatiwa fedha na Benki ya Dunia.
Uwanja wa Kisauni umekuwa ukifanyiwa matengenezo mara kwa mara, ili kukidhi ongezeko la matumizi ya uwanja huo na hasa baada ya kukua kwa sekta ya utalii visiwani humo.

Matengenezo haya yatajumuisha ukarabati wa jengo la uwanja pamoja na utiaji wa uzio katika baadhi ya maeneo ya uwanja huo ambayo yapo hatarini kuvamiwa kwa ujenzi wa nyumba za kuishi. Aidha kampuni itakayofanyia matengezeno uwanja huo Sogea Satom ya Ufaransa imenukuliwa ikisema kazi hiyo itachukua muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu kukamilika.



4 comments:

EDWIN NDAKI (EDO) said...

ni matumaini yangu hiyo kampuni inakuja ikiwa imejizatiti kuanzia vitendea kazi hadi wataalamu sio waanze story mwisho wa siku tuambie hiyo kampuni ilikuwa ya kuchapisha magazeti..

tutafika tu

Kibunango said...

Sio Utani, isije ikawa kama ile Kampuni ya Kichina!

Simon Kitururu said...

Mita zikiongezeka hizo Kisauni itakuwa na uwezo gani? Hivi sasa inaweza kuhimili ndege ngapi?

Kibunango said...

Simon,
Uwanja huu kwa sasa una mita 2,462 katika sehemu ya kutua na kupaa kwa ndege. Ambayo ndio sehemu inayoongezwa, hivyo basi ukarabati utakapokamilika uwanja huu utakuwa na urefu wa mita 3,022.

Hii itatoa nafasi kubwa kwa ndege kubwa kutua katika uwanja huo. Hata hivyo idadi ya ndege ambazo zinaweza kupark katika eneo la uwanja itabaki kuwa ni ile ile ya zamani, kwani sehemu hiyo haipo kwenye matengenezo.

Uwanja huu zaidi ya kutumika kwa ndege za wastani na ndogo, hauna nafasi kwa ndege kubwa kabisa.