Avumae Baharini ni Papa.....
Kwa mara ya kwanza vidagaa baharini vimeanza kujiuliza ni nani mkubwa kati ya Papa na Nyangumi, huku wakiwa wamesahau kuwa avumae bahari ni Papa lakini kubwa lao ni Nyangumi..!
Papa ndie anaye aminika kutamba baharini, kwa mwendo wake wa kasi na mashambulizi ya ghafla tena ya kutisha, kiasi ya kumfanya awe ni maarufu sana baharini.
Hivi karibuni katika vita vya mafahali wawili wa baharini, imeonekana kuwa pamoja na ukubwa wa Nyangumi, Papa bado ni maarufu sana kwa ukubwa katika bahari ya maharamia wa meli hadi kule kwa prez asie tumia ndomu. Hata hivyo wataalumu wa mambo wanasema ni nadra sana kwa vidagaa, vibua, ngisi, pweza, changu,tasi na aina nyingine ya visamaki katika eneo hilo kumwona Nyangumi, hivyo kwao Papa bado ndio samaki/mnyama mkubwa kabisa licha ya kuwepo kwa Nyangumi.
Kama vile haitoshi vidagaa hivyo, ambavyo mara nyingi hukaa mbali na Papa, wameendelea kuhoji ni kwa nini Papa ametumia televisheni ya taifa la wanyama wa baharini,kujinadi kama yeye sio mkubwa kama Nyangumi, wakisahau kuwa Papa hana ubavu kama wa Nyangumi ambae ametumia televisheni yake yenye uwezo wa kuonekana live katika eneo lote avumalo Papa!
Kuna taarifa ambazo sio rasmi kuwa Nyangumi atajaa tena kwenye televisheni yake akipinga madai kuwa yenye ndie mtafunaji wa kwanza wa vidagaa na aina nyingine ya visamaki katika eneo hilo la bahari, huku vidagaa vingine vikifanya mpango wa kwenda kwenye maeneo ambayo Nyangumi amekuwa akivuliwa kwa wingi ili kuweza kujionea samaki hilo lipo la aina gani, na kama inawezekana kuliondoa katika eneo lao la bahari, licha ya madai yake kuwa yupo katika kuwatetea vidagaa na umaarufu wa Papa.
__________________
1 comment:
Kzi nzurinimependa lugha ya picha.
Hakika sisi wengine ni wafugaji sasa tumebaki njia panda..Maana sijui kati ya papa na nyangumi yupi mkubwa?
Labda ningeenda pale feri(mahakamani) wanithibitishie wale wachuuzi wa samaki (takukuru) kwamba samaki yupi ni mkubwa!
Na je ukubwa au udogo wa samaki una athari gani kwa viumbe hai?
mambo yakiwa magumu itabidi tunywe "UJI WA RA AZIZI ingawa una mambo MENGI"
Tutafi tu!
Post a Comment