Saturday, 21 August 2010

Wakimbizi wa Kizenj, karibuni tena Zanzibar


Wale wanzenji wote waliokimbimba Zanzibar kutokana na mtafuruku wa uchaguzi wa mwaka 1995 na mwaka 2000, mnakaribishwa tena Zanzibar.

Zanzibar ya leo ni tofauti sana na ile mliyoikimbia. Sasa kuna makubaliano na kutakuwepo na serikali ya umoja wa kitaifa mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu. Hivyo basi sio sahihi tena kujiita wakimbizi ilhali hali ya nchi ni shwari.

Aidha naiomba serikali ya Uingereza kuwarudisha wazenj wote waliongia nchini humo kwa madai ya ukimbizi, ombi hili ni pamoja na serikali ya Kenya ambako kuna wakimbizi wa kizenj katika mapango huko Mombasa.

Sina shaka kuwa Wazenj wa UK wengi wao wamepata bahati ya kusoma huko na kuwa na taaluma, hili ni muhimu kwa kujenga taifa jipya la Zanzibar... Kule mapangoni sina hakika kama waliweza kupata nafasi ya kujiendeleza.

Cha msingi kwenu wakimbizi wa kisiasa ni kurudi nyumbani, kwani hakuna vujo tena, kura zenu tunazihitaji hali kadhalika maarifa yenu. Hii ajialishi kama ukuweza kufanikiwa huko ugenini.

Karibuni tena nyumbani, tena mjisikie huru kuliko huo uhuru wa kubaguliwa katika nchi za kigeni. Karibuni sana

7 comments:

Anonymous said...

wewe kibwengo yaelekeya hujuwi unachokisema najuwa mikahawa zenj imefungwa kwahiyo njaa inakusumbua kwataarifa yako wakimbizi waliyoondoka zenj hivi sasa ni raiya wa nchi walizokibiliwa wakimbizi waliyokimbiliya Tanganyika wamenyimwa haki yao ya kupewa uraiya kwahiyo kama umekusudiya waliokimbiliya uk wanakuja usiku na mchana walioko tanganyika tutabadilishana nyinyi mtarudi kwenye makaazi yenu ya asili na wazenj watarudi kwenye asilizao sawasawa ama kweli vituko vya zenj mmasai au mdegereko kumkaribisha mzanzibar kwao

Anonymous said...

kibungalo wakimbizi wakirudu na nyinyi wavamizi walowezi mfunge virako kwani hamna nafasi tena kuwagawa na kuwafitinisha wazanzibar katika nchi yao

Anonymous said...

oya msela kibungalo wewe mzenji kwani au ni mmoja wa wavamizi tu wa nchi yetu?

unaijua population ya wanzibar wanaoishi nje ya nchi yao...lol ni wengi sana x 3 ya Watanganyika waliovamia zanzibar....kwa hiyo sisi kabla ya kurudi hapo nyumbani..watanganyika nyote muwe musha ondoka zanzibar, ndio tutapata nafasi ya kuishi bila ya kubanana....si unajua ki island chenyewe kidogo..wapatie habari hii watanganyika wote wanaoishi zanzibar...Peace

Anonymous said...

kibungalo jee watoto wawakubwa tunao wengi naovilevile niwakimbizi kama sisi tofauti yetu na watoto wa wakumbwa sisi tunafanya kweli kama kusoma tunasoma siyo kama wewe na wezako mkisoma hakuna zaidi ya uwadishi wahabari mnapoteza pesa za smz kibungalo znz yetu sote tulikimbiya si kwakutaka tukaacha vilovyetu leo unafanya kejeli wewe dogo nyamaza tukustir kosa letu na imani zakizenj zilipowapokeya wazee wako tukafikiri mtakuwa watoto wa kiungwana kumbe wezi wafazdhila

Anonymous said...

unaona sasa blog yako inachangamka. jibu sasa mapigo hayo.

Kibunango said...

Awali ya yote, jina ni Kibunango na maskani yangu ni pale Kiks...

Cha Msingi wale wote ambao walikimbia Zenj kwa sababu za kisiasa, sioni tena sababu muhimu ya kuendelea kuishi huko ugenini.

Hivyo basi ni vema mkarejea home na kuanza kuijenga Zenj mpya siomjua Mpba au Mmunguja.

Anonymous said...

kibungano mimi mtoto wa shamuhuna baba yangu mzanzibar kida kindaki lakini zenji sirudi bora nifiye ukimbizini kuliko kurudi huko nakijana yoyote aliyesoma na kuona maisha humrudishi bongo yaelekeya umechanganyikiwa wewe zenj hakuna maisha ya kuishi wanadamu mwenye akili zake mambo ya kupigana vikumbo na wamasai unacheza wewe chaooo