Thursday, 13 September 2007

Ni Msimu wa Beer za Mafichoni...Zanzibar


Mwezi wa Ramadhan huko Zanzibar, hubadilisha sura ya kawaida ya visiwa hivyo, aidha pilikapilika nyingi za kawaida huenda likizo ya muda, huku pilika nyingine huchukua nafasi katika kipindi hiki.

Kwa wanywaji wa bia ambao hawafungi, uungana na wananchi wengine ambao wana imani zingine kuendelea kunywa bia, kwa staili ya kujifungia ndani ya nyumba za ulevi....Kwa ufupi katika kipindi hiki cha mfungo, migahawa, hoteli, baa na majumba mengine yote ya starehe hufungwa. Hakuna sheria rasmi ya kufanya hivyo, ila kwa kuwa imekuwa ikifanyika kwa miaka nenda rudi sasa inaonekana ni kama sheria. Na iwapo ukishikwa unakula mchana katika mfungo huu, basi utasekwa rumande na kuachiwa baada ya siku moja au kushitakiwa kabisa!

Miaka kadhaa huko nyuma Beer ilikuwa ikiuzwa katika hotel za serikali tu wakati wa mfungo huu. Tena waliokuwa wanakusudiwa hapo ni watalii tu...! labda na wageni wa serikali ambao wana imani tofauti. Zaidi ya kuuza bia, hoteli hizo pia ndio zilikuwa zikiuza msosi. Hata hivyo mambo sasa yamechukua sura mpya. Baa nyingi huendelea kufanya kazi katika kipindi hiki, zikiuza bia na misosi. Tofauti ya mwezi huu na miezi mingine ni kuwa unywaji ufanyika kwa kujificha, na katika mazingira ya ukimya kabisa, huku wengi wakisubiri king'ora cha kufuturu...!

King'ora kikisharia, kumbi hizo ufunguliwa milango, redio hufunguliwa na kelele za kawaida za kwenye baa huanza kusikika! Hali hii uwepo kwa muda wa mwezi mzima.

1 comment:

Aliko said...

kweli kabisa sasa hivi kona kama sisiem maishara na vijiwe vingine kule jangombe hupata wateja waziada. maanke si bia tuu ambazo huvuta watu ni pamoja na vyakula mbalimbali vya kina mama ntilie mambo kama kuvuta sigara kupanga maswala nyeti na jinsia ya tofauti maanke hadharani unaweza kurushiwa mawe.