Saturday, 13 September 2008

Weekend Njema...
Forodhani bado inaendelea kufanyiwa mabadiliko makubwa ambayo yatawezesha kupatikana kwa huduma bora kwa wadau wote watumiao eneo hilo maarufu sana hapo Zenj... Zaidi hata umiliki wa eneo hilo la historia utabadilika na kuwa chini ya Agha Khan Foundation. Kiutawala kuna mengi ndani ya eneo hilo, kuna migongano kati ya Mamlaka ya Mji Mkongwe, Baraza la Manispaa, Idara ya Mipango Miji, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi na Ofisi ya Waziri Kiongozi.. Hata NGO nazo kwa wakati mmoja au mwingine zimeweza kulitaka eneo hilo, mojawapo ni ZAYADESA...Upande mwingine wafanyabiashara hasa wale wauza vyakula usiku nao udai kuwa hilo ni eneo lao.

Lakini cha msingi eneo hilo linafanyiwa ukarabati katika muda muafaka, na ni ukarabati mkubwa kabisa kufanyika katika eneo hilo. Cha msingi ili eneo hilo liendelee kuwa katika mvuto na kupunguza uharibifu baada ya kufunguliwa tena, ni vema kwa sasa wadau wa eneo hilo wakapatiwa mafunzo juu ya kutunza mazingira ya eneo hilo. Hii isisubiri mpaka uchakavu mwingine utakapotokea. Wote tunajua kuwa "Samaki mkunje angali mbichi" Hivyo hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa sasa kwa kutoa elimu ya utunzaji na matumizi ya eneo hilo kwa wadau wote watumiao eneo hilo kwa njia moja ama nyingine.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

weekend njema nawe pia. Hapo hiyo mishkaki mmmh mpaka mate yananidondoka nimetamani kweli.

kibunango said...

Ukipata nafasi karibu Zenj... ufaidi mishikaki ya samaki,kuku na nyama...iliyotenezwa kwa ubora wa hali ya juu..