Wednesday, 8 October 2008

Mbolea ya Mboji katika mjadala


Waalimu wawili wakuu wa shule ya Msingi za Kahama na Kirumba pamoja na Mwalimu toka shule ya msingi Isenga, wakifuatana na Mratibu wa Mradi wa Tampere - Mwanza wametembelea chuo cha TAMK Tampere kujadili maendeleo ya mradi wa utengenezaji wa mbolea katika shule zao jioni ya leo. Pichani Waalimu hao wakitoa maelezo juu ya mradi huo ambao kwa ufupi umekuwa ni wa mafanikio makubwa.

Aidha wanafunzi wa TAMK walipata kutoa shukrani zao juu ya ushirikiano mkubwa wakati wa uanzishaji wa mradi huo wa aina yake wenye lengo la kuwashirikisha wanafunzi katika utengenezaji wa mboji.



Hadi sasa shule zote tano ambazo zipo kwemye mradi huu zimefanikiwa kuzalisha mbolea hiyo, huku shule ya msingi ya Isenga ikiwa tayali imeanza kutumia mbolea hiyo kwa upandaji wa miti katika shule yao. Mwalimu toka Isenga alisema kuwa mafanikio hayo yameanza kuvuka mipaka ya shule hiyo kwa baadhi ya wakaazi wa karibu na shule hiyo kuanza kutengeneza mbolea ya mboji.

Mipango ya baadae ni kuendelea kutoa elimu ya utengenezaji wa mboji kwa shule nyingi zaidi katika Jiji la Mwanza. Aidha kutoa nafasi kwa wanafunzi na wananchi wa jiji hilo kupitia vikundi kazi kutembelea jiji la Tampere ili kutoa ujuzi wao wa kutengeneza mbolea kwa wakaazi wa jiji la Tampere. Hii itakuwa ni nafasi nzuri zaidi kwao, kwani matumizi ya artificial fertilizer yanategemewa kupungua kwa kasi katika nchi ya Finland kutokana na kuongezeka kwa bei yake kwa kiwango cha asilimia 300.

Kwa upande wa TAMK wanafunzi wameonyesha kulidhika sana na mradi huo kiasi kwamba idadi ya wanafunzi wanaotegemewa kwenda kwenye awamu ya pili ya mradi huo imeongezeka. Hii ni changamoto kwa Jiji la Mwanza kuandaa shughuli nyingi kadili ya idadi ya wanafunzi hao ili kuweza kunufaika vema na utaalamu wao.

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

hiyo ni mbolea nzuri sana. Unajua huwa nalima lima kibustani kidogo hapa. naozesha majani yote lakini inachukua muda mwingi kuoza labda miaka miwili kama hivi

Simon Kitururu said...

Habari poa hii!

Kibunango said...

Yasinta.. mbolea hii ya mboji ni ile inayotokana na bio waste(taka za jikoni) ni nzuri sana na huwa tayali kati ya mwezi mmoja na miezi mitatu

Anonymous said...

Hii ni habari njema lakini Samahani ndugu ila una tatizo la kuto tofautisha herufi L na R. Hatusemi TAYALI ni TAYARI.

Kibunango said...

Shukrani kwa ufahamisho...

Anonymous said...

niliwahi kusikia ati wachina wa tazara walikuwa wakitumia kinyesi cha binadamu kama mbolea. sijui kama ni kweli.

je, unafahamu project yoyote ya kutengeneza bio-gas kwa kutumia kinyesi cha binadamu na wanyama kama ngombe na nguruwe?

Kibunango said...

Sina hakika kuhusu Wachina hao wa Tazara. Ila kinyesi cha binadamu kwa muda sasa kimekuwa kikitumika kwa utengenezaji wa mbolea.

Kuna project nyingi za Bio gas zinazotumia kinyesi cha binadamu, kwa ukaribu unaweza kutembelea Tengeru/Usa river. Hapo kuwa wananchi wengi ambao hutumia bio gas katika kupika na kwa kuwashia taa. Arusha kwa ufupi kuna sehemu nyingi ambazo unaweza kuona jinsi ya utengenezaji wa Bio gas.

Karibu Sana